Menu
 

Habari na Ester Macha,Mbeya.
Umoja wa wanawake na vijana wa  kikrito Tanzania,(YWCA) Tawi la Mbeya  umeonya wanasiasa kuacha tabia ya kuwatumia vibaya vijana na kwamba hali hiyo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa uvunjifu wa amani na kuleta machafu yasiyokuwa na tija hususan katika ushiriki wao  kutoa maoni ya  katiba mpya.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu wa umoja huyo Thabitha Bi. Bughali alipokuwa akizungumza na mwananchi alisema kuwa kwa miaka ya hivi karibuni vijana wengi  na wamekuwa wakipoteza mwelekeo kutokana  na kurubuniwa na hali ya kisiasa  bila kujali haki zao za msingi katika serikali iliyopo madarakani.

"Vijana mnapaswa kutojikita katika siasa bali sasa ni wakati wa kuagalia serikali iliyopo madarakani ina fanya nini katika kuhakikisha mnapata haki sawa hususan elimu,ya msingi sekondari na vyuo nchini"Alisema.

Alisema kuwa ni wakati sasa wanasiasa kutowahusisha vijana katika michakato ya kusimama na kuichafua serikali katika majukwaa kwani  sio wakati wa kuwatumikisha vijana bali ni kipindi cha  kuwajengea uwezo vijana kujikita katika swala zima la elimu ili kuweza kupata ajira za kudumu  na  kutimiza malengo na nia ya serikali katika kuhakikisha  vijana wanaishi maisha bora kwa kila mtanzania.

Aidha alisema kuwa ni wajibu wa kila mtanzania kutambua wajibu wake mahala alipo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika ushiriki wa katiba mpya itakayolenga kujua nini changamoto inayowakabili vijana,walemavu,wajane,wazee na si kuburuzwa na wanasiasa.

"Wananchi tunapaswa kutambua serikali yetu inataka kujua nini kwetu sisi kwani hatuwezi kuingiza siasa katika kutafuta maendeleo ya nchi na kwamba ni vyema kujitokeza kushiriki zoezi zima la kuchangia katiba mpya na kutoa maoni yao hususan sensa ya watu na makazi"Alisema.

Aidha ametoa wito kwa wazazi,walezi  na jamii kwa ujumla kuwafichua watu wanaowaficha walemavu majumbani kwani  wanapaswa  kuwafichua ili kujua haki zao za kimsingi hususan kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi agost 26 mwaka huu hususan kuhakikisha wanapata haki zao za msingi elimu afya na maradhi

Aidha Bi.Bughali pia ametoa wito kwa vijana kuachana  na tabia ya kutumikishwa katika shughuli mbalimbali za kijamii na badala yake kujikita katika elimu ili kuweza kuwa na taifa la wasomi wengi zaidi   na  kuingia katika ushindani wa soko la ajira Nchini..

Post a Comment

 
Top