Menu
 


Tarehe 27 ya mwezi wa tisa ndio ilikuwa birthday ya Rapper toka Marekani kwa jina la Dwayne Michael Carter, Jr alias Lil Wayne kwa kuweza kutimiza miaka 30.

Lakini cha kufurahisha ni kuwa Rapper wa kike toka YMCMB, Nicki Minaj alijipanga na kununua Gari aina ya T- REX CYCLE yenye thamani ya Dollar za Kimarekani $70,000. Hii ni gari yenye matairi matatu ,ni nyepesi sana na ina spidi ya 150mph.

Kwa upande wa bei halisi ya gari ilo ni Dollar za Kimarekani $50,000 , ila baada ya kununua Nicki Minaj aliitengeneza  iwe na muonekano wa Lil Wayne pamoja na kuandika ujumbe nyuma ya gari hio unaosomeka “Nicki Loves Tunechi.”.

Basi gari ilo ndilo Nicki Minaj alimpatia Weezy kama zawadi yake katika siku yake ya kuzaliwa wakati wa sherehe iliyofanyika Alhamis hii.

 
Kwa hisani ya http://baabkubwamagazine.com/

Post a Comment

 
Top