Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Rungwe na Chunya.
Mwananchi Mmoja Mkazi wa Kijiji cha Ipelo,Kata ya Kandete Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya, Mwalisu Kilole (67) amefariki dunia akiwa shambani kwake baada ya kmwili wake kuteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea Septemba 5 mwaka huu majira ya saa 1 usiku wakati marehemu huyo akiwa shambani kwake alipokwenda kulima.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana Yuda Mwasambogole,amesema kuwa alipata taarifa za kifo cha mtu huyo ambapo alipofuatilia alikuta mwili wa marehemu umeteketea kwa moto na mpaka sasa chanzo cha moto huo hakichaweza kufahamika.

Baada ya uchunguzi uliofanywa na madaktari,mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya maziko.

Wakati huohuo Mkazi wa Kijiji cha Ifuko Sifa Pascal Nyerenga amefariki dunia baada ya kutumbukia katika Mto Songwe,Wilaya ya Chunya Mkoani hapa wakati akiogelea.

Marehemu amesadikika kuwa kabla ya kifo chake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kifafa,ambapo mwili wake ulipatika majira ya tatu asubuhi Septemba 5 mwaka huu.

Post a Comment

 
Top