Menu
 

Habari na Ezekiel,Kamanga.
Mwanamke mmoja Vi Matrida Charles(42) Mkazi wa Kitongoji cha Motomoto B,Kijiji cha Motomoto,Kata ya Ruiwa,Welaya ya Mbarali Mkoani Mbeya,anaishi na wanaume wawili kwa wakati mmoja kwa takribani siku nne mpaka hivi sasa.

Tukio hilo la aina yake lililofanywa na mwanamke huyo baada ya kutelekezwa na mumewe wa awali Bwana George Mwasomola anayetoka Kijiji cha Mahango,ambaye ameishi naye kwa mika 25 kabla ya kumtelekeza miaka saba iliyopita naye kukimbilia Mkoani Morogoro na kurejea Septemba 8 mwaka huu.

Baada ya kurejea alimkuta mkewe Matrida akiishi na mwanamke mwingine aitwaye Idd Msongole(50),miaka saba iliyopita katika nyumba ambayo mwanamke huyo alijengewa na mwanae ambaye baba yake alifariki kabla ya kuolewa na mwanamme wake wa sasa anayeishi naye.

Septemba 9 mwaka huu Bwana Mwasomola alimwita mkewe huyo wa zamani nyumbani kwao Kijiji cha Mahango,ndipo mwanamke huyo akamjibu kuwa aje kijijini kwao Motomoto na kumtaka mumewe wa saa Bwana Msongole aondoke hapo nyumbani na alitakiwa kuishi kwa Balozi wa Shina Bwana Mussa Haonga,huku kila mmoja akipata huduma ya chakula,maji ya kuoga na kila mmoja kutembelewa kwa nyakati tofauti.

Baada ya kuona vitimbi hivyo viongozi wa Kitongoji cha Motomoto B ukiongozwa na Mwenyekiti wake Bwana Andrea Mwambije,aliamua kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji Bwana Kassim Mwagala ambaye naye alimtaarifu Afisa Mtendaji wa Kijiji Hussein Mwantanji na baadae Bi Matrida kuulizwa kuwa yupi ni mume wake halali ambapo alijibu kuwa ni Bwana Idd Msongole,ingawa ndiye aliyetolewa nyumbani hapo nakwenda kuishi kwa balozi akimwacha bwana Mwasomola akijivinjari na kuzua gumzo kijijini.

Hata hivyo uongozi wa kijiji umekuwa na wakati mgumu endapo mmoja kati ya wanaume hao atakapo taharuki hivyo umetoa taarifa katika Ofisi za Kata na Kituo cha Jeshi la Polisi Igurusi ili kuchukua tahadhari.

Aidha katika uchunguzi umebaini kuwa Bwana Idd Msongole ambaye anaishi kwa Balozi kwa sasa yupo tayari kusubiri hata mwezi mmoja ili Bi Matrida amalizane na Bwana Mwasomola kuweka saini katika ofisi ya kijiji kuhakikisha usalama wa wanaume hao,licha ya mwanamke huyo kukiri wazi kuwa kwa sasa anependa kuishi na mumewe wa sasa Msongole kwa kuwa mume wake wazamani Bwana Mwasomola alimtelekeza miaka saba iliyopita.

Habari za ndani zinadai kuwa katika sakata hilo uongozi ulimtoza adhabu ya shilingi 100,000 mwanamke huyo,ambapo alilipa shilingi 90,000 na mumewe wa zamani alitozwa shilingi 50,000 na kutakiwa aondoke mara moja.

Wakati hayo yakijiri Bwana Msongole kila asubuhi alikuwa akifika nyumbani kwa mwanamke huyo akitokea kwa Balozi na kuichukua mifugo kwenda nayo machungoni na kurejea majira ya jioni na baadae kuelekea kulala kwa balozi huku Bwana Mwasomola alikuwa akielekea Mahango kwa ajili ya biashara.

****Hatima ya kitendawili hiki kitateguliwa na Matrida mwenyewe endelea kufuatilia mtandao huu******.  

Post a Comment

 
Top