Menu
 

Na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
 JESHI  la polisi Mkoani Mbeya linawashilia wanafunzi  sita akiwemo Mkuu wa Chuo  cha uuguzi   Chimala  Francis Mteja  kwa  tuhuma za kuhamasisha vurugu  zilizopelekea  kuharibu gari la Mkuu wa Wilaya ya  Mbarali Gulamu Hussen Kiffu kuvunjwa vioo,kutoa upepo wa matairi baada ya serikali kufunga chuo hicho kwa kutokuwa na hadhi ya kudaili wanafunzi.
 
Akizungumza Kamanda wa polisi mkoni mbeya.Athuman Diwani alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 11 za jioni baada ya mkuu wa wilaya kuongoza na baadhi ya viongozi wa serikali  hususan kamati ya ulinzi na usalama wilaya kwa lengo la kutaka kujua sababu za chuo hicho kuendelea kufundisha wakati serikali ilitoa agizo kifungwe.

Aidha kamanda  Diwani  amewataja wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni Mkuu wa Chuo  Francis Mtega () steven Mapunda (19) Isaya Katuwa (23)  Lugano Mwalupasya (22) emmanue bukuku (24) na steven Mapunga ambao wanatarajia kufanya mtihani wiki ijayo ya kuhitimu mafunzo ya uuguzi.

Aidha alisema kuwa kutokana na upelezi kukamilika watuhumiwa watano watafikishwa mahakani leo ambapo mkuu wa chuo atafikishwa mara baada ya uchunguzi kukamili
 
Alisema   muda mfupi  kwa  lengo la  kuzungumza na uongozi wa chuo ndipo baadhi ya wanafunzi  walivamia gari la mkuu wa wilaya na kuaza kuvunja vioo kwa kutumia mawe,na kisha kutoa upepo kwa malengo yasiyojulikana.
 
“Tukio hilo lilitokea jana na linaonyesha ni mpango uliokuwa umepangwa na uongozi wa chuo kwani serikali ina malengo mazuri kwa watanzania  na lengo kuu ilitaka chuo hicho kisajiliwe  ili kitambulike serikali na kuweza kutoa wauguzi walio na sifa na kuwawezesha kupata ajira itakayotambulika serikalini”Alisema

“Ni kitu cha kushangaza sana mkuu wa chuo ni mwalimu huyo huyo,mhasibu,na kwamba kulikuwa hakuna sababu ya kufanya vurugu bali  kilikuwa ni kitu cha kutoa vielelezo vya udaili wa chuo na  uchunguzi umebaini chuo hicho kimeanza muda mrefu na tayari  kimeweza kutoa wauguzi katika Nyanja mbalimbali  bila ya serikali kutambua  kama hakijasajiliwa na hakitambuliki ’Alisema.

Aidha diwani ametoa onyo kwa wanafunzi katika vyuo kutojiingiza katika mikumbo isiyokuwa na tija na hivyo kuchangia kuisabishia hasara serikali kutokana na uharibifu uliojitokeza katika vurugu hizo na  kuongeza kuwa watuhumiwa wa takaobainika kuhusika katika vurugu hizo watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
 
Diwani alisewa mpaka sasa wanafunzi wanaoshilikiwa 32 ambapo kati ya hao 5 ndio waliobainika kuhusika na vurugu hizo na wanatarajiwa kufikiswa  mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazowakabili ili sheia ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Akizungumza kwa  njia ya Simu Mkuu wa Wilaya ya Mbarali . Gulamu Hussen Kiffu alikiri kutokea kwa vurugu hizo  zilizotokana na uamuzi wa serikali kufunga chuo hicho  kutokana na kutokuwa na sifa ya kufundisha na kudaili wanafunzi  wa fani ya uuguzi kwani kilikuwa hakina hati ya utambulisho wa usajiri serikalini.

Kiffu alisema kuwa baada ya serikali kutambua tatizo hilo ndipo walipo kumuhita  Mkuu wa Chuo  hicho Francis Mteja katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ambapo aligoma kuhudhuria na kueleza kuwa yeye anaendelea kufundisha ndipo walipolazimika kufika chuoni hapo jana.
 
“Serikali ilikuwa na lengo zuri sana na chuo hicho lakini kutokana na uelewa mdogo ndio imeweza kutokea hali hiyo kwani serikali haiwezi kuvumilia  vyuo kuendeshwa kienyeji wakati huo watu watakaohitimu hapo watapata ajira katika vituo vya afya ,hali hiyo inaweza kuleta madhara kwa watanzania wasiokuwa na hatia kiafya.”Alisema.

Aidha baadhi ya wanachi  Mkoani mbeya wamelaani vikali tabia hiyo na kuitaka serikali kuchua hatua za makusudi kwani kufanya hivyo ni uvunjifuni ya nchi yetu na taifa kwa ujumla kwani kiongozi wa serikali anapaswa kuheshimwa kwani ndio kiungo kikuu katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.


Aidha uchunguzi uliofanywa na mwananchji umeabaini  kuna baadhi ya wananchuo walikuwa wametoka katika mazoezi ya vitendo katika vituo mbalimvali vya afya na wanatarajia kufanya mitihani ya kuhitimu  jumatatu na hivyo kujikuta wakiingia hasara kutokana na chuo hicho kufungwa.

Post a Comment

 
Top