Menu
 


Baada ya jana kutangazwa kuwa balozi wa Pepsi nchini akiwa pamoja na Juma Kaseja, Barnaba amesema uteuzi huo umetokana na kufunzwa vizuri na THT.
“THT ndio source ya mimi kupata hii kitu,” ameiambia Mpekuzi. “Kwasababu wameniteach vizuri, wamenitengeneza vizuri, wamenibrand vizuri, at the end of the day wengine wakaniona.”

Amesema kanuni ya THT ni kumtengeneza msanii anakuwa mkubwa na kumfikisha kwenye sehemu ambayo anaweza kusimama mwenyewe.

“Ni bahati tu, watu huwa wanakaa wenyewe, makampuni yanakaa yanaona nani tumweke nani tumwongeze.

 Kaseja alikuwepo tangu muda, lakini jana kama ulivyoona, sijaingia rasmi lakini ndio nimetambulishwa kama balozi mpya, kuanzia wiki ijayo ntakuwa rasmi kwasababu kuna contract natakiwa nizisign, mikataba ya hapa na pale na makubaliano ya hapa na pale kisha ndo mambo yaendelee like ndo utaona posters, vipeperushi, mabango, matangazo, lakini vitu vingine siwezi kuviweka wazi zaidi kutokana na taratibu zipo kwenye mazungumzo zaidi.

Akizungumzia kazi atakazokuwa anazifanya Barnaba amesema, “mtu kama mimi kwa kazi yangu ya muziki nafikiri ntakuwa nasafiri kwa promotion za muziki, matangazo ya Pepsi, watatumia sauti yangu.”

Hata hivyo amesema hawezi kusema atakuwa analipwa kiasi gani kwakuwa bado wapo kwenye mazungumzo.
 
“Nikiwa tayari nitawaambia kwasababu bado hata contract zenyewe hatujazisaini vizuri.”
 

Post a Comment

 
Top