Menu
 

Na Angelica Sullusi,Mbeya
Vijana waishio katika Jiji la Mbeya wametakiwa kujiunga pamoja pasipo kujali itikadi za dini,ukabila wala vyama vya siasa katika kuhakikisha wanakabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.

Hayo yamesemwa jana na Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mbeya Dk.STEVEN MWAKAJUMILO katika hafla ya kufahamiana ya kikundi cha vijana wa Forest Mpya iliyofanyika katika ukumbi mdogo wa hoteli ya Manyanya eneo la Forest.

Dk.Mwakajumilo alisema kuwa kutokana na changamoto nyingi zinazolikabili taifa vijana hawana budi kujenga mawazo ya kujiajiri kuliko kujibweteka kwa kutegemea serikali itawafanyia kila kitu.

“Kupitia kikundi hiki tuanze kujenga taswira mpya za kutafuta miradi mikubwa ili kuhakikisha kila kijana anajitegemea kiuchumi katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa zima”alisema.
 
Aidha,aliwapongeza vijana hao kwa kubuni mradi wa ufugaji kuku na kuwataka vijana wengine Jijini hapa kuiga mfano kutoka kwa kikundi hicho.

Jumla ya shilingi milioni mbili pamoja na ahadi zilichangwa katika kuimarisha mfuko wa kikundi hicho kwa ajili ya maandalizi ya usajiri.

Post a Comment

 
Top