Menu
 

Na Ester Macha,Mbeya
Matukio ya wivu wa kimapenzi yameendelea kushika kasi Mkoani Mbeya ambapo Mkazi wa Kijiji cha Ivela  kata ya Bara Mkoani Mbeya  Denis Nelson kuuwa kwa wivu wa kimapenzi baada ya kukutwa akifanya mapenzi na mke wa mtu .

Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mmoja aitwaye Maines Fwambo  na siku ya tukio marehemu alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo kwa lengo la kufanya mapenzi.

Wakizungumza na majira mashuhuda wa tukio hilo wambao hawakutaka kutaja majina  yao wamesema kuwa Agosti 29 mwaka huu majira ya saa 4.asubuhi wakati marehemu akielekea nyumbani kwa mwanamke huyo walitokea shemeji za mume wa mwanamke huyo na kuanza kumfuatilia marehemu.

Wamesema kuwa mara baada ya kufika marehemu nyumbani kwa mwanamke huyo  shemeji za mwanamke huyo nao walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkuta marehemu akiwa ndani na kuanza kumshushia kipigo.

Baada ya kuingia ndani walimkuta marehemu akifanya tendo la ndoa  na mwanamke huyo ndipo walipochukua jukumu la kumnywesha sumu na kuanza kumpiga  mwanaume huyo sehemu mbali mbali za mwili wake.

Hata hivyo marehemu alifariki dunia  kabla ya kufika hospitali hospitali ya mission mbozi kupatiwa  matibabu.

Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Diwani Athuman amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wahusika wote wanasakwa na polisi ili waweze kuchukuliwa hatrua za kisheria.

Post a Comment

 
Top