Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Mary Jimmy (55 - 60), Mkazi wa Barabara ya Tatu, Sokomatola Jijini Mbeya amefariki dunia alipokuwa aliabudu katika Ibada ya asubuhi(Morning Glory) kwenye Kanisa moja kubwa eneo la Kabwe jijini hapa Oktoba 23 mwaka huu.

Tukio hilo lilimetokea majira ya saa 1:30 asubuhi ambapo imedaiwa kuwa marehemu alifika kanisani hapo  majira ya saa 12:30 kwa nia ya kufanya ibada ndipo akiwa katika maombi alianguka chini na waumini walifanya maombi bila mafanikio mpaka walipoamua kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa na kuthibitisha kifo chake.

Mdogo wa marehemu ambaye hakupenda kutajwa jina lake kwa madai kuwa si msemaji wa familia alisema kuwa marehemu aliondoka nyumbani akiwa mzima kabisa hivyo kifo hicho kimemshitua mno.

Mwili wa marehemu unafanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Rufaa na mazishi yanataraji kufanyika leo katika makaburi ya Nonde jijini hapa. Marehemu ameacha mtoto mmoja wa kiume.

Tukio jingine Mkazi mmoja wa Iziwa, Jijini hapa Mbwiga Mwalungwe(60), amefariki dunia baada ya kujinyonga nyumbani kwake kwa kutumia waya wa simu Oktoba 24 mwaka huu baada ya marehemu kumpiga mkewe.

Inadaiwa marehemu alimpiga mkewe aitwaye Bi. Taines Mbwiga(45) Oktoba 23 hali iliyompelekea kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini hapa ambapo alipewa PF3 kwa ajili ya kutibiwa na kulazimu kulazwa hospitalini hapo.

Baada ya mkewe kulazwa hospitalini, Jeshi la Polisi lilianza kufuatilia tukio hilo ndipo marehemu alipogundua kuwa anakabiliwa na mkono wa sheria aliamua kuchukua uamuzi mgumu kwa kuchukua waya wa simu majira ya saa 4 kamili asubuhi Oktoba 24, kisha kujinyonga nyumbani kwake.

Aidha polisi walifika eneo la tukio majira ya saa 6:00 mchana na kuuchukua mwili wa marehemu hadi hospitali ya rufaa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hata hivyo hali ya Bi, Taines inaendelea vema ambapo ameruhusiwa kutoka hospitalini Oktoba 2 na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali hiyo.

Kwa upande wake Balozi wa mtaa huo Bwana Chaina Juma amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba anawaachia jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili kupata kiini hasa cha Bwana Mwalungwe kujiua kwa kujinyonga.

Post a Comment

 
Top