Menu
 

 Na DJ SEK BLOGU
Story na Bongo5.COM
 Habari kubwa weekend hii kwenye website, blogs za burudani na mitandao ya kijamii nchini ni kuhusiana na tukio la rapper wa kundi la Nako 2 Nako, Lord Eyez kudaiwa kuhusika kwenye wizi wa baadhi ya vifaa vya gari la msanii mwenzie Ommy Dimpoz.

Habari tulizonazo zinadai kuwa bado polisi wanamshikilia rapper huyo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kwamba tukio hilo lilitokea jana maeneo ya Kinondoni Manyanya.

Pia kuna taarifa kuwa Lord Eyez alikuwa pamoja na kijana ambaye husema ni mtoto wa aliyewahi kuwa rais wa Zanzibar Salmin Amour (ukweli ni kuwa si mwanae bali aliwahi kuishi na familia hiyo) ambao wote wanashikiliwa. Kijana huyo amewahi kuhusika katika matukio mengine kama hayo ya wizi wa vifaa vya magari.

Jana kupitia Twitter, Ommy Dimpoz aliandika, “Mwizi wetu kasema vitu viko chimbo tandale…naona km naota#LordEyesMwiziWaPowerWindow.”

“Kinachoniuma alidhamiria coz gari yangu anaijua na mizinga akinipiga huwa namtoa.”
“Sio mm tu wiki iliyopita alimuibia kerry mfanyakazi wa clouds tv huku akishirikiana na mtoto wa kigogo mkubwa ambae wanavuta nae madawa.”

Tukio hilo limevuta hisia za wengi hususan wasanii wenzie ambao wengi wanashindwa kuamini iwapo rapper huyo amefikia hatua ya kuhusika na matukio ya wizi.

“Hajapatwa na hatia bado lakini mambo ya huu mji yanafahamika na kupata taarifa sahihi ambazo mamlaka huwa zinakwepa kuzifanyia,” aliandika MwanaFA.

“INNOCENT UNTIL PROVEN GUILTY…. But sioni sababu ya @ommydimpoz kumkashifu LORD EYEZ kaka ishu sio ya kweli….but still acha tusubiri,” alitweet Reuben Ndege aka Nchakalih.
Tukio tayari liko mikononi mwa polisi na uchunguzi unaendelea.

Post a Comment

 
Top