Menu
 

Na Greyson Chris Bee Salufu/Chimbuko Letu.
Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Soka ya Tanzania Prisons inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ya Mkoani Mbeya wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka mara tatu eneo la Hare ambapo watu watano wamejeruhiwa, majira ya saa 5 usiku wa kuamkia leo wakati wakielekea Mkoani Tanga kwa ajili ya mechi dhidi ya Mgambo JKT itakayofanyika siku ya Jumamosi Oktoba 27 mwaka huu mkoani hapo.

Akizungumza kupitikia Kipindi cha Bomba Special Show cha Bomba FM redio 104.0MHz kinachorusha matangazo yake kutoka Mkoani Mbeya, Nyanda za Juu  Kusini Kepteni wa Timu hiyo Shaban, amesema gari hilo lilikuwa na jumla ya watu 30 na chanzo cha ajali hiyo imetoakana na gari kubwa la mizigo lililokuwa likija mbele yao kwa mwendokasi na wakati dereva wao alipojaribu kulikwepa gari hilo la mizigo ndipo lilipopinduka mara tatu.

Ameongeza kuwa baadhi ya wachezaji hao ni pamoja na MISANGO MAGAYI, ISA MANTIKA, LAURIAN MPALILE na mwenzao mmoja sambamba na kiongozi wao mkuu wa msafara ndio waliokimbizwa Hospitalini usiku huu kutokana na hali zao kuwa tete na Jeshi la Polisi lilifika mapema katika tukio hilo.

Sikiliza hapa Kepteni wa timu hiyo akizungumza moja kwa moja kupitikia Kipindi cha Bomba Special Show cha Bomba FM redio 104.0MHz:-

Post a Comment

 
Top