Menu
 

MBUNGE VITI MAALAM MBEYA DR.MARY MWANJELWA AKIWA HOSPITlLI YA FISI BAADA YA KUPATA AJALI


HILI NDILO GARI T 671 ABM TOYOTA HILUX (RANGER) ALILOKUWEMO MBUNGE MARY MWANJELWA LIMETEKETEA LOTE KWA MOTO


PICHA NA MBEYA YETU NA KALULUNGA BLOG


A
UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni huo ndio msemo pekee ambao naweza kuutumia katika kukujuza yaliyotokea katika ajali mbaya ya Mbalizi Mbeya Vijijini.

Wakati wengine wakiendelea kuokoa majeruhi wengine wamejikuta wakifanya tofauti na vile ilivyotegemewa pale kijana mmoja alipojitoa mhanga na kuingia katika mmojawapo wa waokoaji na kutaka kumchomolea fedha “ waswahili huita mshiko”.

Asalale kijana huyo ambaye hajafahamika jina mpaka mauti yanamkuta katika tukio hilo alikwidwa na mashuhuda wa ajali hiyo na kupewa kichapo cha mbwa mwizi wa kuku.
Kwa hisani ya blog ya malafyaleleo
 
Mkuu wa mkoa Mbeya Abas Kandoro akiangalia ajali iliyotokea Mbalizi Mbeya


  Hiace nambari T 587 AHT ikiwa imeharibika kabisa baada ya kugongwa na Lori na kisha kupinduka na kusababisha kifo cha abiria kadhaa akiwemo Askari wa Jeshi la Polisi PC Samson
Lori nambari T 814 BTC na tela nambari T 911  BUV likiwa limeteketea kwa moto baada ya kupinduka

Habari na Ezekiel Kamanga.


Baadhi ya watu waliioshuhudia ajali hiyo, walisema kuwa lori hilo la mafuta lilifeli breki na kuanza kutelemka kwa kasi katika mlima huo, ambapo liliyagonga magari matatu ukiwamo Hiace yenye namba za usajili T 587 AHT.

Kwa upande wake, Muuguzi wa Hospitali ya Ifisi, Sikitu Mbilinyi  alisema mbunge Mwanjelwa analalamika zaidi maumivu katika sehemu ya mgongoni  na miguu  sawa na dereva wake ambaye naye analalamikia miguu na amepasuka sehemu ya kichwani na kubainisha kwamba wamepokea maiti mbili.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandolo ametoa taarifa rasmi baada ya kutembelea Hospitali za Rufaa na Ifisi na kusema kuwa watu 10 wamefariki dunia na watu 25 wamejeruhiwa na kwamba 17 wamelazwa Rufaa na wanane wamelazwa Ifisi pia maiti nane zipo Rufaa na mbili Ifisi.
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi kufika katika Hospitali hizo ili kutambua maiti na majeruhi na amewashukuru wauguzi kwa huduma nzuri na Jeshi la zimamoto na Polisi kufika kwa wakati katika tukio hilo.

 HIVI NDIVYO MAAFA YALIVYO
 HIVI NDIVYO HILI GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI
 MAMIA YA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO MBALIZI
 HIVI NDIVYO GARI HILI LILIVYO PINDUKA NA KUWAKA MOTO BAADA YA AJALI
 HII NI GARI NYENGINE AMBAYO PIA ILIWAKA MOTO BAADA YA KUGONGANA 
 FIRE WAKIWA WAMEWAHI ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUZIMA MOTO HUO
 ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WAKIWA WAMEFIKA ENEO LA TUKIO AMBAPO MAGARI HAYO YAMESABABISHA VIFO VYA WATU 10
 WATU WAKIWA WAMEONGEZEKA KUSHUHUDIA TUKIO HILI LA AJALI
 HUU NDIO MUONEKANO WA GARI HILI LIKIWA LIMEUNGUA LOTE
 HAYA NI MABAKI YA GARI HILI AMBALO NALOLILIUNGUA LOTE
WANANCHI MBALIMBALI WAKIWA WANASHUHUDIA AJALI HUKU WENGINE WAKIWA WANAENDELEA KUOKOA WALIOPATA AJALI
KIKOSI CHA FFU NAO WALIKUWEPO SAMBAMBA KATIKA KUHAKIKISHA ZOEZI LA UOKOAJI LINAENDA KIKAMILIFU.
PIA KATIKA ENEO HILI  MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWAALIKUWEPO NDANI YA PICK UP ILIYOUNGUWA MOTO, KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO HUO.
PICHA  NA HABARI : MBEYA YETU BLOG

Post a Comment

 
Top