Menu
 

meli mpya zanzibar azam sealink marine Meli Mpya ya Abiria ya Azam Marine yawasili Zanzibar

Meli mpya ya abiria inayomilikiwa na Azam Marine yatia nanga rasmi katika bandari ya Zanzibar. Meli hiyo imetokea Ugiriki na itaaza kazi baada ya kumaliza taratibu zote za Kisheria za Baharini, kukaguliwa na taasisi husika, na kupata leseni ya kusafirisha abiria na mizigo. Meli hiyo ina uwezo wa kuchukua abiria 1500, mizigo, na magari 270 kwa wakati mmoja.
Meli hiyo itafanya safari kati ya Unguja, Pemba na Dar-es-Salaam hivi karibuni ili kuondoa tatizo la usafiri wa maji kati ya visiwa vya Pemba na Unguja ambako kuna tatizo la usafiri tangu kutokea kwa ajali ya MV Spice Islander, na baadhi ya meli kufutiwa leseni za kusafirisha abilia kutokana na meli hizo kutokuwa na hali ya kuridhisha ya kusafirisha watu.
Wananchi wamefarijika kuona tatizo la Usafiri kati ya Unguja na Pemba limepata ufumbuzi baada ya kuona meli hiyo katika bandari ya Zanzibar na kutumaini kuwa huduma yake itakuwa nzuri na ya kuridhisha. Wananchi hao pia wamewataka wafanyabiashara kupunguza nauli ili kila mwananchi aweze kumudu huduma hiyo na wasiwe katika biashara zaidi kuliko kutoa huduma kwa wananchi wa hali ya chini ambao hutegemea usafiri huo.
Meneja wa Azam Marine, Hussein M Said amesema meli yao itakuwa katika kutoa huduma zaidi kuliko biashara ili kuona kila Mwananchi anafaidika na huduma zao, na wataweka nauli za bei nafuu kwa wananchi.

Post a Comment

 
Top