Menu
 

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Iwambi, darasa la tatu Kervin Patrick (8) jinsi ya kiume amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu katika bomba ya maji nje ya nyumba yao.

Tukio hilo limetokea Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa 5 kamili usiku wakati wazazi wote wa mtoto huyo Bwna Patrick Mwakapalila(52) na Bi Subira Patrick(30) wakiwa hawapo nyumbani na kwamba baba mzazi akiwa na mwanae wa kiume aitwaye Joshua Patrick(10) waliondoka majira ya saa 3:30 kuelekea mjini.

Aidha Baba wa mtoto huyo alipigiwa simu na mtu mmoja kwamba arejee nyumbani na yeye pasipo kuchelewa alirejea na kumkuta mwanae amejinyonga katika bomba la maji kwa kutumia kamba ya viatu na chini kukiwa na ndoo, ambapo kifo hicho kimezua maswali mengi kwani kimo cha mtoto ni zaidi ya futi mbili na nusu na urefu wa kamba hali inayotia shaka kuwa mtoto huyo alichukua uamuzi huo yeye mwenyewe.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Ivwanga Bwna Chonde Kalisto amethibitisha tukio hilo la kusikitisha na kwamba yeye alipokea taarifa kutoka kwa Balozi wake Bi Esther Mahenge ambapo walitoa taarifa polisi ambapo walifika eneo la tukio kisha kuuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi na hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.

Post a Comment

 
Top