Menu
 

* Marehemu adaiwa kufariki baada ya kula nyama ya tambiko.
* Mwingine akumbwa na wazimu baada ya kukata mti.

 ********
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Watu wanne wakazi wa Kijiji cha Wimba Mahango, Kata ya Ruiwa, Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamenusurika kifo baada ya wananchi wenye hasira kali kutaka kuwazika wakiwa hai, baada ya kudaiwa kutaka kumuua Wiston Nsanja(52), kiushirikina baada ya marehemu kudaiwa kula kwa pupa nyama ya tambiko mapema mwezi Julai mwaka huu.

Watu hao wamefahamika kwa majina ya Julius Sibela, Julius Nsalanga(Bundala), Rajab Benyanga(Putu) na Jailos Mdanga(Kazi), ambao wote wanadaiwa kumloga kishirikina marehemu baada ya kukiri mbele ya wakazi wa kijiji hicho kabla ya kifo chake na ndipo alianza kuugua mwezi Julai na kutibiwa katika Hospitali mbalimbali bila mafanikio hadi kifo kilipomchukua Oktoba 5 mwaka huu majira ya saa tatu usiku.

Aidha kabla ya kifo cha Wiston wananchi hao wakiwa na hasira walianza kumshaka mtuhumiwa mmoja baada ya mwingine na kufanikiwa kuwakamata wawiliambao ni mzee Benyanga na Sibela na kabla ya kuchukuliwa hatua zozote, Afisa Mtendaji wa kijiji Bwana Naftali Sengele alipewa taarifa na wasamaria wema na yeye kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji Bwana Wiston Kazimoto.

Kufuatia taarifa hizo viongozi hao hawakusita kutoa taarifa Ofisi ya Kata ya Ruiwa na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata Bwana Zephania Mgaya, kwa kushirikiana na Mugambo wa kijiji walifanikiwa kuwanasua mikononi mwa wananchi wazee hao na kuwasalimisha katika Ofisi ya kata na baadae kuwapeleka Polisi katuo cha Rujewa kwa usalama zaidi huku wazee wengine Nsalanga na Mdanga wakitokomea kusikojulikana.

Mnamo majira ya asubuhi ya Oktoba 6 mwaka huu, wananchi waligoma kumzika marehemu wakidai azikwe na waliosababisha kifo chake yaani waze wanne ambao ni Mzee Nsalanga, Benyanga, Sibela na Mdanga kauli ambayo waliitoa katika Mkutano wa hadhara nyumbani kwa marehem, pia ilidaiwa wazee hao ndiyo waliosababisha mwanamke mmoja kukumbwa na ugonjwa wa wazimu baada ya kukata mti unaodaiwa kutumika katika matambiko.

Hata hivyo wananchi walikubali kumzika marehemu baada ya Afisa mtendaji kuwakamata watuhumiwa na kuwapeleka polisi na wananchi kudai hawatakiwi teba kijijini hapo.    
 

Post a Comment

 
Top