Menu
 

Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Charles Tizeba (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TRL, kutoka kushoto ni Bw Maez, Meneja Mahusiano wa TRL, Bw.Hassan Shaban, Meneja Masoko wa TRL (kushoto kwa Naibu Waziri) na Bi.Elizabeth Msemwa, Afisa Masoko (wa pili kutoka kushoto).(Picha na Maktaba ya http://www.mot.go.tz)
********
Hawa Mathias,Mbeya.
 NAIBU Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles  Tizeba amemwagiza mkandarasi aliyeshika zabuni ya  ujenzi wa mradi  wa uwanjwa wa ndege wa kitaifa wa Songwe jijini Mbeya kurudia tabaka la pili kwenye sehemu ya kutua ndege  kwani lililopo halijakidhi   kiwango  na  kupelekea ucheleweshaji wa mradi huo kuanza kutumika .

Kauli hiyo alitoa jana wakati alipokuwa akikagua mradi wa uwanja huo na kueleza kuwa utaanza kutumika  pindi yatakapokamilika majengo ya hali ya hewa,usalama wa unga na jengo la abiria na waongoza ndege  ambayo yapo katika hatua za mwisho na serikali haitosubiri mpaka takaba hilo likamilike na hasara za marudio ya tabala zitakuwa za mkandarasi na si serikali .

"Uwanja  huo utawanufaisha watazania zaidi ya milion 1 na utaanza kutumika hata kama mkandarasi ajaweka tabaka la pili na kwamba serikali haitoweza kuvumilia wananchi wake kushindwa kuutumia uwanja huo huku wakiwa na shauku kubwa na kwamba hasara za ukarabati wa tabaka lingine  ni za mkandarasi na si serikali"Alisema.

Aidha alisema kuwa mkandarasi anapaswa kufanya jitihada za haraka kuhakikisha  anajitahi kukamilisha  na kwamba endapo kama atafanya uzembe atajikuta akiingia hasara mara mbili kwani ukarabati wa uwanja wakati ndege zinatua unakuwa na gharama kubwa.

Alisema kuwa kutokana na hilo ndege zitaendelea kutua ili kuruhusu shughuli mbalimbali za kijamii kuendelea  na  kuongeza tija ya ukuaji wa uchumi hususan kwa wanambeya ambao wanahitaji kujua hatma ya kukamilika kwa mradi huo.

"Tabaka lililowekwa kwenye sehemu ya ndege kutua limechakachuliwa kwa kiasi kikubwa ni lazima serikali iliangalie hilo  kwani huo ni sehemu ya miradi ya wananchi "Alisema.

Tizema alisema kuwa kusuasua kwa  mradi huo  kulitokana na kutokuwepo kwa uelewano baina ya mkandarasi na mhandisi  mshauri na hivyo  kama serikali tumeyaweka sawa  kufanya mabadiliko ya mkandalasi na hivyo tumefikia hatua nzuri ya maelewano na uwanja huo utaanza kukamilika desemba mwaka huu.

Aidha kwa upande mwingine aliwataka wakurugenzi wa viwanja vya ndege kuangalia uwezekano wa kujenga mabwawa ya maji kulingana na mahitaji ya abiria na kwamba wasijenge kwa kufanya makadilio .

"Mnapaswa  kuangalia idadi ya watu wataotumia uwanja huo na viwiane   na mabwawa ya maji na hivyo katika hilo mtakuwa mmefanikisha malengo mliyokusudia"Alisema .

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa viwanja vya ndege Nchi Suleima Suleiman alisema kuwa hizi ni changamopto zinazojitokeza na kwamba katika hilo watahakikisha mkandarasi anamalizia kazi yake kulingana na mkataba ili uwanja uanze kutumika desemba mwaka huu.

"Nina hakika kazi itakamilika na wananchi kuanza kutumia uwanja wao na kwamba ni jitihada tu zinahitajika na msukumu wa mkandarasi ili kuweza kukamilisha mradi huo.

Post a Comment

 
Top