Menu
 

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
JESHI  la polisi  Mkoani  Mbeya  limefukuza kazi Askari wake Enock Daffa (22)  kwa tuhuma  za kufanya  mapenzi  na mtuhumiwa wa kike  mwenye umri wa miaka 25 katika kituo cha polisi cha mji mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani hapa.
Kwa mujibu wa  kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya  Athuman Diwani   askari huyo alitenda kosa hilo Novemba 21,2012 na kwamba  mtuhumiwa aliyefanya naye mapenzi alikuwa  anakabiliwa na kosa la wizi.
Kamanda Athumani alisema kuwa mbali ya kufukuzwa kazi askari huyo tayari amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Mbozi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvuliwa na jeshi la polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.
Kamanda huyo alitopa wito kwa askari polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za jeshi la polisi kama mwongozo unavyowaagiza ili kuinda maadili ya jeshi la polisi ambacho ndicho chombo kinachotumika na wananchi katika kuzisimamia sheria.
Akizungumzia tukio hilo baba mzazi  wa askari huyo alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha kiungwana ambaco kimetia fedheha familia yake lakini pia kwa jeshi la plisi ambalo limepewa dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali zake.
Wakati  huo  huo  katika  kijiji cha malangali barabara ya Mbeya Iringa Wilaya ya Mbarali gari yenye namba za usajili DFP 7322 aina ya Nissan Patrol lilimgonga mtembea kwa miguu na kusababisa kifo chake papo hapo.
Alisema kuwa marehemu bado haujafamika  na mwili umehifadhiwa katika hospitali ya Chimala Mission na kwamba juhudi za kuutambua mwili wa marehemu na mahali anapotoka zinaendelea.

Post a Comment

 
Top