Menu
 

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya
MAHAKAMA ya hakimu mfawidhi  Mkoa  wa Mbeya  imeahirisha  Kesi inayomkabili mwekezaji wa shamba la Mpunga la Kapunga Rice Project lililopo Wilayani Mbarali ya kuharibu mazao  ya wakulima kwa sababu ya kukosekana mkalimani  wa lugha ya kiingereza  na Kiswahili.
Mwezi February 2012 Serikali ilimfikisha mahakamani mwekezaji huyo katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kwa makosa mawili ya kula njama na kutenda kosa kuharibu mai za Wananachi na kusababisha hasara ya zaidi ya shs 800 milioni.
Iidaiwa mahakamani hapo kuwa mwekezaji huyo alitenda kosa kati ya Januari 12 hadi 14 mwaka huu ambapo alimwaga sumu katika mashamba  hekari 489 .5  ya wananachi  zaidi ya 154 wa kijiji cha kapunga kwa kutumia ndege  kunyunyuzia dawa.
Watuhumiwa wa kesi hiyo ni pamoja na Meneja wa shamba Walder Vermaak,Afisa ugani Serger Berkker na Rubani wa ndege Andries Daffe wote raia wa Afrika Kusini.
Akiahirisha kesi hiyo hakimu mfawidhi wa mahakama ya Mkoa Michael Mteite alisema kuwa kutokana na kukosekana  kwa mkalimani wa lugha Kiswahili na Kiingereza anaihairisha kesi hiyo hadi January 7 hadi 10 mwaka 2013 itakaposiklizwa kwa mfululuzo.
Alisema katika siku hizo za kesi mashahidi 40 watatoa ushahidi wao ambapo kila siku ya kesi watasikilizwa mashahidi 10 na kwamba ili haki itendeke ni lazima apatikane mkalimani.
Awali akieleza mahakamani hapo mwendesha mashitaka wa Serikali Christina Joas alisema kuwa upande wa mashitaka unategemea kuleta mashahidi 154 na vielelezo viwili ikiwa ni pamoja na ramani ya eneo la tukio na taarifa ya halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
Katika kesi hiyo Wakili wa utetezi Ladslaus Rwekaza aliioma mahakama kumkabidhi majina ya mashahidi na vielelezo hatua iliyopingwa na hakimu kwa madai kwamba vielelezo atapatiwa lakini siyo majina ya mashahidi.

Post a Comment

 
Top