Menu
 

Na Bosire Boniface, Garissa

Polisi katika Mkoa wa Kaskazini Mashariki ya Kenya wanachunguza mauaji ya mjumbe mwandamizi wa kamati ya polisi jamii ya Wajir yaliyotokea siku ya Jumatano (tarehe 16 Novemba).

Issa Aalim, ambaye hayumo katika picha, alisaidia polisi kufichua dafina ya silaha kwenye Makaburi ya Ahmed Liban mwezi Oktoba. [Na Bosire Boniface/Sabahi]

Watu wasiojulikana wenye silaha walimpiga risasi Issa Aalim, aliyekuwa na umri wa miaka 40, ndani ya nyumba yake katika kitongoji cha Halane mnamo saa 1 jioni kabla ya kukimbia kutoka eneo la tukio, mkuu wa polisi wa Wajiri James Mutungi aliiambia Sabahi.
 
"Aalim alipigwa risasi mbili kichwani na moja kifuani," Mutungi alisema. "Alifariki hapo hapo."

"Hatuwaachi al-Shabaab au wafuasi wao katika kuhusika na mauaji haya kwa sababu marehemu alikuwa na nafasi kubwa katika vita dhidi ya siasa kali wilayani," alisema. "Wakati huo huo, hatuachi kufikiria sababu nyingine."

Kamishna wa Jimbo la Wajir Naftali Mungathia alisema kuwa Aalim alikuwa mjumbe wa Kamati ya Polisi Jamii ya Wajir ambaye aliwasaidia maafisa katika kushughulikia masuala ya usalama mjini.

Post a Comment

 
Top