Menu
 

 
Picha hii haiendani na picha tukio lakini picha hii pia wananchi walikuwa wakifanya uokoaji baada ya kijana mmoja kudumbikia chooni na kufa papo hapo. 
Na.Gabriel Mbwille, Mbozi
 

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la TIENA MWAZEMBE mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa kijiji Hangomba kata ya Bara wilayani Mbozi mkoani Mbeya  amenusurika kufa baada ya kutumbukia chooni wakati akifanya mapenzi huku mumewe akiwa maututi chumbani.

Habari za uhakika kutoka kijiji hapo zinadai kuwa mwanamke huyo licha ya kuwa mke wa mtu alikuwa anafanya ngono chooni na WASI MGALA wakati mumewe akiwa ndani anaumwa na kwamba alidumbukia choo baada ya banzi alilokuwa amekanyaga kukatika wakati wanafanya tendo hilo.

Mwanamke huyo alidumbikia kwenye choo chenye urefu wa futi 17 na kwamba baada ya kudumbukia, mwanaume aliyekuwa naye chooni wakifanya ngono alikimbia na kumwancha mwanamke huyo akipiga kelele za kuomba msaada ndipo wananchi walifika na kufanikiwa kumtoa ndani ya shimo na kukimbiza kwenye dula la madwa linalomilikiwa na muuguzi LEONARD NZOWA ambaye alitoa huduma ya kwanza kabla ya kumfika katika hospitali ya Mbozi Mission.

Hata hivyo mume wa mwanamke huyo SAIKI GODFREY KAROTI amesema kitendo kilichofanywa na mkewe ni cha uzalilishaji na si cha uungwana.

Post a Comment

Michael Minja said... 6 November 2012 at 17:09

Duh hii balaa na hiki choo kilikuwa kinatumika ama.

Chimbuko Letu said... 12 November 2012 at 15:54

Yap kaka choo kilikuwa kinatumika na kina futi 17 aisee balaa kaka

 
Top