Menu
 

 Marehemu Mariam Khamis enzi za uhai wake
Huu ndio usafiri wetu wa mwisho pindi tuondokako duniani ambapo dada yetu Mariam Khamis ameutumia siku ya leo kuelekea makaburini
Mamia ya watu walijitokeza katika mazishi ya muimbaji mahiri wa Taarab nchini Mariam Khamis maarufu kama Paka Mapepe aliyefariki juzi wakati akijifungua. Mariam alifariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo mtoto wake alisalimika.
Mazishi hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu wa aina mbalimbali wakiwemo wasanii wengine wa muziki wa Taarab.
Miongoni mwa wasanii waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Mzee Yusuph na mke wake Bi Leila, Nyota Waziri, Bi Hindu na wasanii wenzake wa kundi la TOT.

 Mwili wa marehemu Mariam Khamis ukiwa unaelekea makaburini mapema leo
 Mamia ya watu walio jitokeza kumsindika dada Mariam kwenye nyumba yake ya milele
 Mume wa marehemu Mariam Khamis akiingia ndani ya kaburi tayari kwa kumzika mkewe pembeni yake ni baba mkwe wake
 Tayari kwa kupokea mwili wa marehemu pindi uingizwapo ndani ya kaburi
 Mwili wa marehemu Maraiam Khamis ukiingizwa ndani ya kaburi
 Mazishi yakiendelea ndani ya kaburi
 Tayari dada Mariam kashazikwa hapo zoezi la kufukia na mchanga likiendelea
 Mwanamuziki wa Taarab Thabit Abdul naye akiiendelea na zoezi la kufukia kaburi la dada Mariam Khamis
 Na hii ndio nyumba yake ya mwisho dada Mariam Khamis ambayo ataishi maisha yake yote
 Kaburi la marehemu dada Mariam Khamis likiwa katika muonekano ambao tayari lishafukiwa
Mume wa marehemu Mariam Khamis akiwa haamini kuwa mkewe hayuko naye tena duniani kiukweli alichokuwa akikiongea hapo pembeni ya kabuli ungekuwepo wewe rafiki yangu sidhani kama ungeweza kuvumilia lazima ungelia pole sana kaka HAJI KIJUNGU mbele yake nyuma yetu.
Mume wa marehemu Mariam Khamis aliporudi nyumbani tu kutoka makaburini alimtafuta mwanaye huyo mtoto unayemuona mwenye tisheti yenye mistari alipomuona tu akaangusha kilio cha nguvu. Mungu awatie nguvu.
---
Mariam alikuwa muimbaji wa kundi la taarab la TOT na enzi za uhai wake aliwahi kuimbia katika makundi mbalimbali ya taarab ambayo ni pamoja na East Africa Melody, Zanzibar Stars na 5 Stars.
Marehemu Mariam Khamis ameimba nyimbo nyingi zinazofanya vizuri katika muziki wa Taarab zikiwemo ‘Huliwezi bifu’, ‘Raha ya Mapenzi’ na ‘Ndo basi tena’.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pepa peponi.


Picha kwa hisani ya Shakoor Jongo

Post a Comment

 
Top