Menu
 

Na Ester Macha 
Serikali ya Tanzania ilitangaza sera ya Kilimo Kwanza kama njia maalumu ya kitaifa ya kuongeza kasi ya kuleta mapinduzi ya kilimo nchini na kuinua pato la wakulima Kwanza inajumuisha mikakati inayolenga katika kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili kilimo chetu na kutumia fursa lukuki tulizonazo kujiondolea umaskini wa kipato.
Azima ya Kilimo Kwanza ilibuniwa chini ya Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) ambalo ni mfumo wa mashauriano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye mwenyekiti wa Baraza hilo.
Licha ya nchi yetu kuwa na hekta milioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo, ni asilimia 23 tu ndiyo inayotumika. Kuna hekta milioni 29 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na maji ya kutosha yapo lakini ni asilimia moja tu iliyo chini ya umwagiliaji.
Aidha, licha ya Tanzania kuwa na maziwa na mito yenye maji ya eneo la kilomita za mraba 62,000, ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi wenye urefu wa kilomita 1,424 na kilomita za mraba 223,000 za ukanda maalumu wa kiuchumi baharini (Exclusive Economic Zone), lakini maji hayo mchango wake kwa pato la taifa na la mtu mmoja mmoja bado ni hafifu .
Moja ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba wanawake waliopo  vijijini  ni ugumu wa maisha uliopo na hivyo kulazimika kujikita zaidi katika kilimo ili waweze kuondokana na hali duni ya kimaisha iliyopo miongoni mwao.

Ili kuhakikisha kuwa wanaondokana hali ngumu ya kimaisha wanawake waliopo vijijini wamekuwa nguzo kuu ya kilimo kuliko wanaume kutokana na na wao kuwa walezi wa familia katika nyumba zao.

Hivi karibuni mwandishi wa makala haya alitembelea katika kata ya Ijombe wilaya ya Mbeya mjini kuona hali halisi ya maisha ya wanawake hususani suala la kilimo ambapo ilionekana kuwa wanawake na watoto wanaendelea kunyanyasika kutokana na badhi ya wanaume kutumia mwanya huo kusafirisha mazao mijini na fedha  ambazo zinapatikana baada ya kuuza mazao  hutumia kwa  anasa Ili kila mwananchi aweze kuishi vizuri na  familia hakuna budi  mazao yanayolimwa.

Wakizungumza wanahabari wanaharakati wa mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP) kijijini hapo leo baadhi ya wanawake wa kata hiyo ya Ijombe wamesema kuwa kukosekana kwa masoko katika kata hiyo ndiko kunapelekea wao na watoto kuendelea kunyanyasika katika mgawanyo wa kipato kinachotokana na mavuna wanayoyapata .

Zuwena Mwakyoma na Atuganile Mwasanga wakazi wa kata hiyo ya Ijombe wamesema   kuwa pamoja na kuwa wakati wa kuandaa mashamba kwa kulima na kutunza mazao hayo hadi yanafikia wakati wa kuvunwa ila ikifika wakati wa mavuno wanaonyanyasika zaidi ni wanawake na watoto huku wanaume wao wakitumia nafasi hiyo kujineemesha mijini .

Zuwena anasema kuwa wakati kata hiyo ya Ijombe ikiwa ni moja kati kata zinazoongoza kwa kuzalisha mazao mbali mbali ya kibiashara ila bado serikali haijaweza kuwakomboa wakulima hao kwa kujenga soko la mazao ambalo litawasaidia wakulima wa kata hiyo kuuza mazao yao na kunufaika na kilimo .

“Leo tumekuwa tukishuhudia jinsi ambavyo sisi wanawake na watoto tunavyonyanyasika na kilimo na kushuhudia baadhi ya wanawake wakinyanyasika kwa waume zao kuongeza wanawake wakati wa mavuno kutokana na wao kuwa wasimamizi wakuu wa mazao hayo ….wamekuwa wakiyasafirisha kwa usafiri wa mikokoteni hadi mjini na huku wakiuza pesa zote wanatumika katika pombe na kuhonga wanawake”.

Hivyo anasema njia pekee ya wanamke na mtoto wa pembezoni mwa miji kuweza kukombolewa ni serikali kuweka utaratibu wa kujenga masoko katika kata hiyo na kata nyingine ambazo zipo pembezoni na miji .

Huku Atuganile akidai kuwa mbali ya baadhi ya wanaume wa kata hiyo kuendelea kuwanyanyasa wakati wa mavuno kwa kuwaongezea wanawake ama wapenzi katika nyumba zao ila bado hata madalali wamekuwa ni kikwazo kikubwa kwani wamekuwa wakifika na kununua mazao yakiwa mashambani .

Anasema kuwa madalali hao wamekuwa wakifika kununua mazao katika mashamba hayo hata kabla ya kuvunwa na sehemu kubwa ya wanaoathirika na mfumo huo wa madalali ni wanawake wajane ambao hawana uwezo wa kutafuta masoko wala kupata fedha za kusafirishia mazao hao na hivyo kukubali kuuza mazao yao kwa bei yeyote ile .

“Kuna baadhi ya kaya ambazo zinaongozwa na mama na baba mwenye moyo wa upendo katika familia yake zimekuwa zikinufaika na kilimo kutokana na kuuza mazao kwa ushirikiano na pesa hutumika kwa matumizi mazuri ila baadhi ya kaya suala la masoko ni kilimo endelevu”.

Pia anasema suala la ushuru limeendelea kuwa kero kutokana na serikali ya wilaya kuwatoza ushuru mara mbili mazao yakiwa shambani na pindi yanapopelekwa sokoni Uyole .

Deus Mwambaje mkazi wa kijiji cha Iwalanje kata hiyo ya Ijombe akijibu madai ya wanawake hao alisema kuwa si wanaume wote ambao wamekuwa wakinyanyasa wake zao wakati wa mazao na kuwa badhi ya kaya zimekuwa na ushirikiano kwa kulima pamoja na kuuza kwa utaratibu mzuri ila badhi ya kaya zimekuwa zikiongoza kwa migogoro na kesi wakati wa mavuno kutokana na wasimamizi wa familia hiyo ambao ni wanaume kuwa na mfumo dume kwa kuuza mazao na pesa kuhonga wanawake mjini.

"Hili ni tatizo kubwa kwa baadhi ya familia kwani inaonyesha ni jinsi gani wanaume ambavyo wamekuwa wanyanyasi wakubwa katika familia zao huku wakisahau kuwa walezi wakuu wa wa familia ni wanawake ni muhimu wanawake nao wakapewa kipaumbele"anasema mwanaume.

Anasema kuwa pamoja na kwamba yeye ni mwanaume lakini vitendo ambavyo vimekuwa vikitokea katika vimekuwa ni vikwazo kwake na kuonyesha kuwa wanawake ni watu wa kuonewa kila wakati,mazao yanalimwa kwa ushirikiano kwa pamoja lakini unashangaa unakuta kipindi cha mavuno ugomvi unakuwa mwingi ndani ya familia.

Mkazi mwingine Bi. Yusta Mwambula anasema kuwa suala la kunyanyaswa kutokana na mazao kwa wanawake wa eneo hilo ni kitu cha kawaida ,kwani hata familia zilizo nyingi zina migogoro mingi kwani ikifika kipindi cha mavuno mwanaume anavuna  mazao na kuuza na kuondoka zake hivyo kwa ujumla hali ni mbaya.

Hata hivyo alidai kuwa pamoja na kuwa kata hiyo inaongoza kwa kulima nyanya, njegere ,viazi ,karoti na vitunguu pamoja na mazao mengine ya biashara ila hakuna soko hata moja.

Afisa biashara wa wilaya ya Mbeya Castro Temihanga alithibitisha madai ya wanawake hao wa kata ya Ijombe kuwa ni kweli kata hiyo mbali ya kuongoza kwa uzalishaji ila hakuna soko na kuwa jitihada za Halmashauri kuzungumza na watu wa SIDO ili kusaidia kujenga soko eneo hilo zinafanyika.

Post a Comment

 
Top