Menu
 

Na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Watoto watatu wa familia moja wameteketea kwa moto uliotokea majira ya saa 2 na dakika 15 usiku Novemba 7 mwaka huu, katika Kitongoji cha Buswema, Kijiji cha Ilundo, Kata ya Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Baba mzazi wa watoto hao Nuru Sambo(31), amewataja watoto hao walioteketea kwa moto kuwa ni pamoja na George Nuru(9), Mevis Nuru(4) na Winnie Nuru(2) wote kwa pamoja walikuwa wamelala chumbani wakati mama yao mzazi Bi. Sifa Asagwile(27), alikuwa amekwenda kumchukua mtoto mwingine Dontisia Nuru(6) aliyekuwa kwa Bibi yake aitwaye Kipesile.

Baba wa watoto hao amesema kuwa wakati wa tukio yeye na mkewe walikuwa hawapo na alipokuwa anarejea nyumbani alikutana na kundi la watu waliokuwa wakielekea nyumbani kwake na wengine kumpa pole asijue kilichotokea na alipofika nyumbani alikuta alikuta nyumba ikiteketea na wanawe wakiwemo ndani ambapo walifariki papo hapo.

Nyumba hiyo ilikuwa imeezekwa kwa nyasi na mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijaweza kufahamika, ingawa kuna tetesi kuwa huenda moto huo ulisababushwa na kiberiti kilichowashwa kabla ya watoto hao kulala.

Aidha, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilundo Bwana Jairo Mpakama amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba mazishi ya watoto hao yatafanyika Novemba 8 mwaka huu, majira ya saa 8 mchana na kuhudhuriwa na wananchi kutoka vijiji mbalimbali waliokuja kushuhudia tukio hilo la kusikitisha.


Tukio jingine Meck Laiton Mbegesi(34) mkulima na mkazi wa Kitongoji cha Utyegu Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, mkoani hapa ameuawa na mtu au watu wasiofahamika kwa kukatwakatwa na mapanga maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Mwenyekiti wa mtaa wa Viwandani, Kijiji cha Matelemehe Bwana Fidelis Dominicus Pelela, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mazishi yamefanyika Novemba a7 mwaka huu kijijini hapo baada ya uchunguzi wa Daktari/.

Mdogo wa marehemu Bwana Emmanuel Manyuki Laiton(28), amesema marehemu alirejea nyumbani usiku majira ya saa tatu usiku Novemba 6 mwaka huu baada ya kutoka katika biashara zake eneo la kilaabuni na baadae aligongewa mlango na watu waliofika hapo kwa kutumia pikipiki kisha kumchukua marehemu mita kadhaa kutoka nyumbani hapo kisha kumpiga mapanga kichwani, masikioni na mdomoni ambapo alivuja damu nyingi na kusababisha kifo chake papo hapo.

Hata hivyo mwili wa marehemu ulikutwa mita kadhaa kutoka nyumbani ambapo ulitambuliwa na wapita njia  na kutolewa taarifa Ofisi ya Kijiji na kisha kutambuliwa na mdogo wa marehemu Bwana Laiton, ambapo taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio na kuuanza uchunguzi kuhusiana na tukio hili.

Baadhi ya wananchi wamedai kuwa tukio hilo huenda likahusishwa na ulipizaji kisasi kwani uhai wake marehemu alikuwa akijihusisha na vitendo vya wizi na kusababisha kero kijijini hapa.

Post a Comment

 
Top