Menu
 

Mtoto wa miaka mitatu na nusu Abiud Moses Mwanyingili mkazi  wa kijiji cha Mponela wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kung'atwa na nyuki alipokuwa akicheza na wenzie kijijini hapo Desemba 13 mwaka huu majira ya saa nane mchana.

Katika tukio hilo kundi la nyuki halikuweza kufahamika limetokea wapi, mbali ya kusabaisha kifo hicho pia nyuki hao wamesababisha kifo kwa Ester Kasebele miaka 6 ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi mkoani hapa.

Aidha Mwenyekiti wa kijiji cha Mponela Bwana Laniwelo Mwampashi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mazishi ya mtoto huyo yamefanyika kijijini hapo baada ya kufanyiwa uchunguzi na Daktari wa hospitali ya wilaya hiyo.

Wakati huohuo mlinzi aliyefahamika kwa jina moja la Mwanzembe ameuawa kikatili na mtu au watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, karibu na lango la hospitali ya wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoani hapa Diwani Athumani amwthibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi lake linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na taarifa zaidi zitatolewa na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Post a Comment

 
Top