Menu
 

DAKTARI wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,Paul Kisabi (32), anayetuhumiwa kwa kupokea rushwa ya sh 200,000


Brandy Nelson,  Mbeya
DAKTARI  wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Paul Ngiga amefikishwa katika mahakama ya Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kushawishi na kupokea Rushwa ya sh. 200,000 kutoka kwa ndugu wa mgonjwa.

Akisoma mashitaka mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa Mbeya Francis Keshenye Nimrodi Mafwele  akishirikiana na Joseph Mulebya alisema kuwa mshitakiwa alitenda kosa Desemba 19,2012  katika bar ya Victory.

Alisema kuwa mshitakiwa anakabiliwa na makosa mawili moja likiwa ni la kufanya ushawishi na la pili ni kupokea rushwa ya shilingi 200,000 kutoka kwa ndugu wa mgonjwa ambapo Taasisi ya kupambana na  kuzuia rushwa ilipoweka mtego wake na kufanikiwa kumkamata.

Ilidaiwa  na mwendesha mashaitaka huyo kuwa mnamo  desemba 18,2012 mshitakiwa  aliomba kiasi hicho cha fedha kutoka kwa ndugu wa mgonjwa aliyefahamika kwa jina la Meshack Mwakilambo kwa ni ya kumsaidia kumhudumia mgonjwa wake.

   Mwendesha mashitaka  Mafwele  alisema kuwa kosa hilo ni kinyume cha sheria kanuni ya adhabu  cha makosa ya jinai kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2007 ambapo  ni kifungu cha 15 kifungu kidogo cha kwanza (a).

Hakimu wa mahakama ya haklimu mkazi Mkoa wa Mbeya Francis Keshenyi alisema mahamani kuwa dhamana ipo wazi na kwamba kesi hiyo italetwa mahakamani hapo hadi Desemba,27,2012.

Mshitakiwa baada ya kusisomewa mashitaka hayo alikanusha kutenda kosa hilo na mshitakiwa yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana  na alidhaminiwa na mdhamini mmoja kwa gharama ya sh 500,000.

Post a Comment

 
Top