Menu
 

 Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39), anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(16) jina lake limehifadhiwa. akiingia mahakamani leo mbele yake ni mke wake na mtoto wake aliyezaanae ambao sura zao tumefunika.
Bwana Yussuf Hamad anaetuhumiwa kuzaa na bintie akitaka kumpokonya kamera  mwandishi wa gazeti la majira Rashid Mkwinda ili asimpige picha.
Jamaa kuona amezidiwa akaamua kujifunika na shati lake huku akitoa maneno makali kuwa nyie waandishi mmekosa cha kuandika mmeona hii ndiyo habari hakuna habari nyingine? alihoji mtuhumiwa huyo.
Huyoooo anatoka nje ya mahakama.

Sasa anavaa kofia yake ili watu wasimtambue huku akisema nifuateni niwaonyeshe kazi
Njooni sasa huku kashika jiwe.
Kuona anazidi kufuatwa akaamua kuondoka mahali hapo huku  akiwa na jiwe lake mkononi


Akina mama wanamsindikiza kwa kumzomea mtuhumiwa huyo.(Picha na Mbeya Yetu)

Habari na Ezekiel Kamanga.
 Kesi  inayomkabili mkazi wa Isanga Jijini Mbeya Bwana Yusuph Hamad  ya kuzini na mtoto wake kisha kumpa ujauzito na kujifungua imeendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya Desemba 6 mwaka huu.

Kesi hiyo namba 154 ya mwaka 2012 imesikilizwa na Hakimu Gilbert Ndeuruo na Mwendesha mashtaka Achirey Mulisa, akimwongoza motto kutoa ushahidi katika mahakama hiyo iliyofurika watu lukuki.

Mtoto huyo ambaye jina lake linahifadhiwa aliiambia mahakama kuwa Baba yake Bwana Yusuph alikuwa anamlazimisha kufanya mapenzi huku akimtishia kwa kutumia silaha haramu ya Panga akidai kuwa atamuua endapo atapiga kelele au kumwambia mu yeyote.

Kutokana na kitendo hicho binti huyo mwenye umri wa miaka 16, aliibeba mimba na kujifungua motto wa kike Septemba 21 mwaka huu katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.

Bwana Yusuph aliachana na mkewe Bi. Regina Simonmwaka 2008 ambapo walifanikiwa kupata watoto wanne ambao ni Zainab, Yasin, Yahaya na binti huyo mkubwa aliyemlazimisha kufanya naye mapenzi.

Binti huyo aliiambia Mahakama kuwa baba yake alimwingilia mara nyingi na baada ya kugundua ana ujauzito alimwambia mama yake na kutoa taarifa kwa Balozi wa Mtaa na kasha taarifa kuzifikisha Polisi ambao walimkamata na kumfikisha mahakamani kwa kosa la kuzini na motto kifungu cha sheria cha 158(i)(a) kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Aidha Baba mzazi alionekana kushindwa kuuliza maswali ya msingi hali iliyofanya mahakama kuangua kicheko huku wanawake wakiangua kilio kutokana na ukatili aliofanyiwa motto huyo.

Hata hivyo kesi imeahirishwa hadi Desemba 10 mwaka huu, ambapo upande wa mashtaka utaleta mashahidi wengine na akikutwa na hatia atakabiliwa na kifungo cha maisha.

.

Post a Comment

 
Top