Menu
 

Na Esther Macha, Mbeya
  ILI kila Mwanamke aweze kuondokana na hali duni ya kimaisha hakuna budi kwa kila mmoja wao aweze kujituma kufanya kazi za mikono ambazo zitakuwa mkombozi kwao.

Katika kuhakikisha hilo bado kumekuwepo na changamoto  kubwa kwa wanawake hususani waliopo vijijini ambao bado wanahitaji msaada wa kupata elimu ya ujasiliamali ili nao waweze kuachana na dhana ya utegemezi.


Ili kuona hilo linafanikiwa mashirika mbali mbali yasiyokuwa ya kiserikali yamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa yanawakomboa wanawake ambao kwa kiasi kikubwa bado wanahitaji elimu ya ziada.


Lakini baadhi ya maeneo wanawake wamekuwa na mfumo dume kutokana na waume zao kutotaka wafanye shughuli yeyote kwa kudai kuwa wao ni watu wa kuhudumia familia majumbani lakini si kufanya kazi za kimaendeleo.


Matokeo ya wanawake kuacha  kutojishughulisha na kazi yeyote ni ugumu wa maisha  na kuanza kunyanyaswa na waume zao kwa madai kuwa wanasubiri kuletewa tu  hali ambayo huathiri uchumi wa mwanamke  huyo kwa kiasi kikubwa .


Katika  kuhakikisha wanawake  wanaweza Mwanamke Mmoja ambaye ni mkazi wa Dodoma Mjini Bi.Recho Mwasajone  maarufu kwa jina la (Mama Peter )ambaye anajishughulisha na biashara ya mafuta ya Ubuyu , Sabuni , Rosheni ya Ubuyu,Jamu pamoja na  unga wake wa Ubuyu.


Bi. Mwasajone anasema kuwa biashara ya bidhaa hiyo alianza  mwaka 2011 akiwa na Dada yake Aitwaye Upendo baada ya kupata semina  ya ujasiliamali kutoka Shirika la Viwanda vidogo vidogo Tanzania (SIDO) lililopo Mkoani Dodoma.


“Nikiwa katika mafunzo haya nilijifunza jinsi ya kutengeneza Mafuta ya Ubuyu , Sabuni, Unga wake, Roshen tukiwa wajasiliamali wengi tu wanawake wa Mkoa wa Dodoma kwani  tuliona njia pekee ya kujikomboa ni kujifunza ujasiliamali”anasema Mama Peter.


Bi . Mwasajone anasema kuwa kutokana na Mti wa Ubuyu kutowahi kuwa tiba lakini baada ya kupata mafunzo kutoka Sido sasa jamii imekubali kuwa Ubuyu ni tiba nzuri kwa binadamu ambapo nchi za jirani wamekuwa wakinunua kwa wingi bidhaa hiyo hasa nchini China kutokana na kuona matokeo mazuri.


Hata hivyo Mjasiliamali huyo anatoa kilio chake kwa wafanyabiashara wajanja  ambao wamekuwa wakifika Mkoani hapo na wengine kutoka hapo hapo Mkoani Dodoma kuchakachua bidhaa hiyo hasa mafuta ambayo wamekuwa wakichanganya mafuta ya alizeti ili waweze kupata faida kubwa.


“Hili kama sisi wajasiliamali linatuumiza sana kwani baada ya kufika mikoani kwao huanza uchakachuaji huo wa mafuta na sisi kama wajasiliamali tumekuwa tukilalamikiwa jna wateja wetu kuwa  bidhaa zetu mbona syo zenyewe wanazotumia siku zote”alilalamika Mama huyo.


Hata hivyo anasema kuwa uchakachuaji huo umekuwa ukifanyika kwa mafuta ya ubuyu ambayo wanaona kuwa ni rahisi kuchanganya na mafuta mengine kwa bidhaa zingine wanajaribu lakini wanashindwa.


Anasema kuwa watu waofanya hujuma hiyo lengo lao ni kuharibu  biashara ya wajasiliamali , na pia hawana ujuzi wowote ambao wameupata kutoka SIDO , na kwamba wsengi wa wafanyabiashara  wamekimbilia biashara hiyo bila kujua utengenezaji wake kikubwa ni kujikimu kimaisha tu.


Hata hivyo amewataka wajasiliamali wanaokuja  kununua bidhaa hizo kuacha kuchakachua mafuta  hayo kwani huo ni uchumi  wa kimataifa ambapo nchi za jirani  wamekubali kuwa ni tiba nzuri ambayo wameona mafanikio yake.


Akizungumzia sababu ya kukimbilia biashara hiyo Mjasiliamali huyo anasema kwamba wengi maisha yao ni magumu hivyo wanaona wakifanya biashara hiyo wataweza kuendesha maisha yao.


Hata hivyo Bi. Mwasajone alitoa wito kwa wanawake ambao hawajishughulishi  na biashara kuwa wajiunge na vikundi  kwani  kila Mkoa  kuna vikundi  vya ujasiliamali ambavyo vimekuwa ni mkombozi kwa wanawake wanyonge.


“Nawasihi wanawake Wenzangu tuache kuwa tegemezi kwa waume zetu kwani hakuna kinachoshindikana kikubwa ni kujituma tu katika maisha  yetu ili yaweze kusonga mbele tusibaki tu kusubiri  kuletewa na waume zetu “anasema Mama Peter.


Aidha Bi.Mwasajone anaongeza kuwa  kama wajasiliamali wa Dodoma hawana  wa bidhaa hivyo wapo tayari kuwasaidia wanawake wenzio kwenda Dodoma kununua bidhaa hizo kwenda nazo Mikoani kuuza ili kuondokana na na hali duni ya kimaisha.


Aidha Mjasiliamali huyo anasema kutokana na biashara hiyo  ameweza kuboresha maisha yake  kwa kutoka nyumba ya kupanga  na kujenga nyumba yake mwenyewe ambayo anaishi mpaka sasa,pamoja na kusomesha watoto wake wanne.


Anaeleza kuwa  kufuatia mafanikio hayo  amekuwa  tegemezi  katika familia kwa kusaidia misaada ndugu wa karibu .


Akizungumzia Ndoto ya Maisha yake Bi.Mwasajone anasema  kuwa ni kusaidia jamii ya watoto wanaoishi katika  mazingira magumu kwani Mkoa wa Dodoma umeathirika sana na watoto wanaoishi katika mazingira magumu
.
Anasema kuwa  Mkoa wa Dodoma  umekuwa na watoto wengi  kutokana na jamii yenyewe kutokuwa makini na maisha ya  kutafuta fedha na kubaki kuomba misaada badala ya kujituma kufanya kazi.


Mjasiliamali  huyo anasema kuwa changamoto kubwa waliyonayo kama wajasiliamali ni ukosefu wa vifaa vya utengenezaji wa bidhaa hizo, hivyo wameiomba serikali  kuboresha  mafuta  ya ubuyu  ili yawe na usimamizi mzuri katika  utengenezaji  wa bidhaa.


Anasema kuwa serikali ikitusaidia uboreshaji wa biashara hii kwa wajasiliamali itaweza kusaidia kuinua maisha ya wanawake hasa waliopo vijijini ambao hawana msaada wowote wa kujiimarisha kiuchumi .


Hata hivyo anasema kuwa  kampuni yao hiyo ambayo inajulikana kwa jina la M.S.Bao Bao Seed oil Dodoma .


Wakizungumza na gazeti hili baadhi ya watumiaji wa mafuta hayo Bi.Estilina Adamu Mkazi wa Mbeya anasema kuwa alianza kutumia mafuta ya Ubuyu na Sabuni zake mwaka huu mwezi januari  na kuona mafanikio yake kwani awali alikuwa akisumbuliwa na tumbo ambalo mpaka sasa ameweza kupata nafuu.


“Binafsi haya mafuta  mimi yamenisadia sana nilikuwa nasubuliwa sana na maradhi ya tumbo, kichwa na maradhi ya kuwashwa “anasema .


Pichani Mwandishi wa gazeti hili Bi.Esther Macha akipata maelezo kutoka kwa Mjasiliamali kutoka Mkoani Dodoma Bi. Recho Mwasajone anayejishughulisha na ujasiliamali wa kutengeneza bidhaa za Ubuyu.

Post a Comment

 
Top