Menu
 


Expendable two iliyowashirikisha action movie stars kibao wakiongozwa na Sylvester Stalonne (Rambo), Jean Claude Vanndamme, Jet-Li, Arnold ShwazNiger, na wengine, imekumbana na tatizo la kisheria. 
 
Waandaaji na wawezeshaji wengine wanakabiliwa na mashtaka yanayotokana na scene ambayo haikwenda sawa na kupelekea mtu mmoja kupoteza maisha na mwingine kujeruhiwa vibaya.

Mtu mmoja anaejulikana kwa jina la Nuo Sun alijeruhiwa vibaya katika mlipuko ambao ulisababisha kifo cha muigizaji Kun Liu, ambapo kwa mara ya kwanza familia ya marehemu iliiburuza mahakamani ‘Expendable 2’ wakidai fidia mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha kiasi cha dola za marekani 25,000.

Taarifa za hivi karibuni zinasema Nuo Sun ambae alijeruhiwa vibaya na kupelekwa jijini Munich huko Ujerumani kwa matibabu akiwa chini ya the best specialist amewafungulia mashtaka waandaaji na washiriki wengine wa movie hiyo.

Katika mashitaka hayo yenye kurasa 12 Sun amedai kuwa, “mlipuko na similar extra-hazardous activities vilisababisha tukio la hatari juu ya rubber boat wakati wa kushoot sehemu ya pili ya filamu hiyo October 27, 2011.

“Kwa uzembe wa moja kwa moja wa washitakiwa, kutojali, na matendo kinyume na sheria, mlalamikaji aliumia na kupata majeraha katika afya yake, uwezo wa kufanya kazi, mshituko wa kiasi kikubwa na majeraha katika mfumo wake wa fahamu, shingo, kichwa, mwili, mikono na miguu, majeraha yote haya yanaweza kuwa ya kudumu, na majeraha haya yamesababisha na yanaendelea kusababisha madhara katika fahamu zake na mwili wake kwa ujumla. Hivyo mlalamikaji anadai fidia .” Haya ni baadhi ya maandishi yanayopatikana kwenye faili la mashtaka lenye kurasa 12.

Akiwakilishwa na Robert M. Klein, Sun anadai fidia ya hasara ya kipato chake kwa wakati uliopita, uliopo na ujao. Lakini pia anadai fidia ya jumla zaidi ya $25,000, gharama za matibabu ya wakati uliopita, uliopo na hata baadae, gharama za kuendesha kesi na mengine ambayo mahakama itaamua.

Baada ya mlipuko huo ulioua mmoja kati ya actors wa movie hiyo na kumjeruhi vibaya Sun, uongozi na watayarishaji wa movie hiyo walitoa tamko kuomba radhi na kuwaitakia pole familia ya marehemu na vilevile kuendelea kusapoti kwa karibu sana familia na kumhudumia Sun akiwa hospitalini.

Hata hivyo Sun alikanusha kauli iliyotolewa na waandaaji hao kuwa Jet-Li alikuwa pia karibu na mlipuko huo, na kusema hakuna star yoyote aliyekuwa karibu na mlipuko huo.  

Post a Comment

 
Top