Menu
 WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO
MNAMO TAREHE 18.12.2012 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO MBALIZI TARAFANI BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA.  GARI  NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU  DENIS S/O FRANK,MIAKA 23,MKINGA,BIASHARA MKAZI WA MBALIZI, NA KUSABABISHA KIFOCHAKE PAPO HAPO . CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI.MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO. JITIHADA ZINAENDELEA KUMTAFUTA MTUHUMIWA NA GARIKAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI  WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI NA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WANYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO DEREVA HUYO AZITOE ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.


WILAYA YA MBOZI - KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
MNAMO TAREHE 18.12.2012 MAJIRA YA SAA 15:30HRS HUKO KIJIJI CHA ICHENJEZYA WILAYA MBOZI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1.VISCUS S/O SICHOLE, MIAKA 40, MNYIHA, MKULIMA2.ELINA D/O MBAGULE, MIAKA 60, MNDALI, MKULIMA 3. HURUMA D/O KAYUNI,MIAKA 30,MNDALI MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ICHENJEZYA WAKIWA WANAKUNYWA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA 4 .WATUHUMIWA NI WANYWAJI  WA POMBE HIYO.TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE MAHAKAMANI.KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI  WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI KOSA LA JINAI, PIA NI HATARI KWA AFYA YA MNYWAJI.


WILAYA YA CHUNYA KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
MNAMO TAREHE 18.12.2012 MAJIRA YA SAA 18:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KIGAMBONI  KIJIJI CHA MKWAJUNI  WILAYA CHUNYA MKOA WA MBEYA . ASKARI POLISI WAKIWA DORIA  WALIMKAMATA ABDALAHA S/O NDEGE ,MIAKA 70,MSONGWE,MKULIMA MKAZI WA KIGAMBONI-MKWAJUNI  AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA 5 . MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO .TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI  WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI KOSA LA JINAI PIA NI HATARI KWA AFYA YA MNYWAJI.
Signed By
[JACKOB KIANGO - SP]
Kny:KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Post a Comment

 
Top