Menu
 

 Na Esther Macha, Mbarali

WAKULIMA wa Kata ya Chimala Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya wamepatiwa mikopo ya kilimo na trekta ndogo (powertiler) yenye thamani zaidi ya sh.444.8 na Benki ya CRDB tawi la Mbeya ili iweze kuwasaidia kuboresha kilimo cha mpunga .

Imeelezwa kuwa  wakulima waliopatiwa mikopo  hiyo ni wale ambao ni  wale ambao ni wanachama wa  akiba na mikopo cha Chimala (Chimala bank Saccos limited) waliojiungua ili kuweza kusaidiwa mikopo.

Mikopo hiyo imetolewa jana na meneja wa Benki  ya CRDB Tawi la Mbeya Bw.Lucas Busigazi kwa wakulima na kwamba makabidhibiano hayo yalifanyika jana kwenye ofisi cha benki hiyo ya Chimala Saccos.

Bw. Busigazi alisema benki hiyo imetoa Powertila aina ya Kubota 38 pamoja na mikopo ya kilimo pamoja na hundi kwa wakulima hao, meneja  na kuwataka wakulima hao kuhakikisha wanaitumia ipasavyo mikopo hiyo ili kuona kila mmoja ananufaika na mikopo hiyo sanjari na kuirejesha mikopo hiyo kwa wakati uliopangwa.

Alisema kuwa benki ya CRDB kwa kuwa inatambua umumhimu kwa kutaka kuona mkulima analima kilimo chake kwa muda mwafaka pamoja na kuona anakuwa na maisha mazuri ndio maana hawachoki kuendelea kuwakopesha wakulima hao mara kwa mara ambapo benki hiyo imeanza kutoa mikopo hiyo tangu mwaka 2004.

“Sisi kama benki tunambua kuwa wakulima ndio wadau na wateja wetu muhimu sana ndio maana hatuchoki kuendelea kuwapatia mikopo mbalimbali ili kuona mnakuwa na maisha mazuri” alisema .

“Tunajua kuwa wakulima kupitia benki yenu ya akiba na mikopo ya chimala Saccos limited, mmekuwa wakopaji wazuri lakini vilevile mmekuwa walipaji wazuri jambo ambalo linatufanya tuendelee kuwa na mahausiano mazuri baina yetu tangfu mwaka 2004 hadi leo hii, hivyo tunaomba muitumie ipasavyo hii mikopo ili muone faida zake”alisema Meneja huyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa benki hiyo ya Chimala  Saccos,Bw. Alphonce Micheal, aliishukuru benki hiyo kwa kuendelea kuwapatia mikopo mbalimbali na kusema kuwa tangu benki hiyo ianze kuwakopesha mwaka 2007 wakulima wengi wameweza kuboresha maisha yao.

“ Tunaishukru sana benki ya CRDB kwa kuendelea kutupatia mikopo ikiwa ni sehemu ya kutaka kuona mkulima anakuwa na maisha mazuri, na kwamba tangu tuanze kuwa mahusiano mazuri na CRDB wengi wetu tumweza kufanikiwa kwa kuboresha kilimo na maisha yetu kwa ujumla wake”alisema Bw.Micheal.

Post a Comment

 
Top