Menu
 

Na Shaban Kondo.
Klabu ya AC MILAN ya nchini Italia inapewa nafasi kubwa ya kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji kutoka nchini humo na klabu ya Man City ya nchini Uingereza Super Mario Balotelli.

AC Milan inapewa nafasi kubwa ya kufanya hivyo baada ya kuhusishwa na muda mrefu na harakati za usajili wa mshambuliaji huyo ambae kabl ya kuelekea nchini Uingereza alikua akiwatumikia Inter Milan ambao ni mahasimu wakubwa wa The Rossoneri.

Katika baadhi ya vyombo vya habari imeelezwa kwamba uhamisho wa Super Mario Balotelli utaigharimu klabu ay Ac Milan kiasi cha paund million 17 ambacho ni ada yake ya uhamisho kutoka nchini Uingereza na kurejea nyumbani.

Hata hivyo bado taarifa hizo zimeeleza kwamba AC Milan watatoa kiasi hicho cha fedha kama ada ya usajili wa Mario Balotelli sambamba na kumuachia kiungo kutoka nchini Ghana Kevin-Prince Boateng ili ajiunge na man city.

Kabla ya makubaliano hayo kufikiwa uongozi wa klabu ya Man City ulikua umetangaza kuwa tayari kumuuza mshambulaiji huyo mwenye umri wa miaka 22, kiasi cha paund million 22 ambacho kilitumika wakati akisajiliwa mwaka 2010.

Uthibitisho mwingine ambao unaonyesha safari ya Super Mario Balotelli ya kurejea nyumbani huenda ukawepo katika kipindi hiki, ni kauli iliyotolewa na wakala wake ambapoa mesema kuna baadhi ya mambo yameshakamilishwa mpaka sasa na wakati wowote habari zitabadilika.

Mino Raiola wakala wa mshambuliaji huyo mwenye sifa ya utukutu ameyasema maneno hayo baada ya kukanusha fununu za usajili wa mchezaji wake kuelekea nchini Italia kwa kipindi kirefu kilichopita.

Wakati huo huo makamu wa raisi wa klabu ay Ac Milan Adriano Galliani usiku wa kuamkia hii leo alijitamba katika baadhi ya vyombo vya habari huku akisema wanaamini dili la kumsajili Mario Balotelli lipo katika asilimia 99.5 na mipango zaidi ingefahamika hii leo.

Katika hatua nyingine meneja msaidizi wa klabu ay Man city David Platt alipoulizwa na waandishiw a habari wakati wa mkutano wa kuzungumzia mchezo wa ligi utakaochezwa kesho dhidi ya QPR, amesema hajui lolote juu ya suala hilo lakini anachofahamu muda wa usajili bado upon a laweza kutiokea lolote.

Hata hivyo David Platt amesema anachotambua kwa sasa ni kwamba Mario Balotelli ni mchezaji halali wa klabu ya Man city.

Post a Comment

 
Top