Menu
 

BASI LA NGANGA LILILOKUWALINATOKEA MBEYA KWENDA DSM LIMEPINDUKA ENEO LA IMEZU  MBEYA AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA MBILI ASUBUHI ABIRIA MMOJA AMEFARIKI PAPO HAPO NA ZAIDI YA MAJERUHI 40 WAMEPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA ABIRIA ALIYEFARIKI AMETAMBUWA KWA JINA LA ENOCK LWILA MKAZI WA MAMA JOHN MBEYA NA NIMFANYABIASHARA MWANJELWA
BAADHI YA WAKAZI WA IMEZU WAMESEMA AJALI HIYO IMESABABISHWA NA MWENDO KASI 

MWILI WA MAREHEMU ENOCK LWILA  UKIWA UMELAZWA CHINI KUSUBIRI WANA USALAMA KUJA UCHUKUA
MAREHEMU ENOCK LWILA AMEKUTWA NA ZAIDI YA SHILINGI MILION 15 KATIKA SOKSI NA KWENYE MIFUKO YAKE YA SURUALI INASEMEKEANA ALIKUWA ANAENDA DSM KUNUNUA BIDHAA MBALIMBALI ZA DUKANI KWAKE
HAPA WANAUSALAMA WAKIHESABU PESA WALIZOZIKUTA KWENYE MWILI WA MAREHEMU ENOCK HUKU WANANCHI WAKISIMAMIA KWA MAKINI ZOEZI HILO LA KUHESABU HIZO HIZO PESA ZAIDI YA SHILINGI MILION 15  ALIKUWANAZO MAREHEMU 

TAARIFA KAMILI YA KUHUSU AJALI HII TUTAWALETEA BAADAE


Basi la kampuni ya Nganga linalofanya safari zake Mbeya kwenda Dar es salaam limepata ajali Januari 20 mwaka huu hii katika kijiji cha Imezu na kusababisha kifo cha mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Enock Lwila Mkazi wa Mama John Jijini Mbeya na majeruhi 48 ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hosptali ya Rufaa Mbeya.Basi hilo lenye namba za usajili T.431 AVU likiendeshwa na Bwana Alex Elias mwenye umri wa miaka 40 lilipata ajali majira ya saa mbili za asubuhi na uchunguzi wa awali umebaini kuwa ajali hiyo imetokana na mwendo kasi.

PICHA KWA HISANI YA KAMANGA

Post a Comment

 
Top