Menu
 

Moja ya duka ambalo lilianza kuwaka moto mida ya saa tatu usiku kutokana na hitirafu ya umeme likiwa na baadhi ya nguo zilizoungua kwa moto huo maduka hayo yapo jirani na kituo cha afya cha Ruanda jijini Mbeya

HABARI KAMILI.


Moto unaodaiwa kuwa umesababishwa na hitilafu ya Umeme jana umeunguza maduka mawili jirani na soko jipya la Mwanjelwa ambapo inaelezwa kuwa moto huo ulianzia chumba cha Mwakibibi na kuteketeza duka lote.Akiongea na mwandishi wetu mmoja wa waathirika wa moto huo Zuberi Ngairo amesema moto huo haukuweza kuleta maafa makubwa kutokana na ushirikiano uliotolewa na wananchi eneo la tukio.Aidha ametoa pongezi kwa wananchi kuhakikisha moto unadhibitiwa huku sanjari na kuwathibiti watu wenye nia ya kuiba pindi panapotokea majanga ya moto.Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa moto huo umeteketeza maduka yanayomilikiwa na Zuberi Ngairo na Limited Sanga duka linalothaniwa kuwa ndipo moto ulianzia.

Post a Comment

 
Top