Menu
 


Asteria Jailosi Chambulia mkazi wa kitongoji cha Totowe kati kata ya Totowe wilayani Chunya mkoani Mbeya amejikuta akipoteza sehemu ya mdomo wake baada ya kufumaniwa na mume wa mtu.


Tukio hilo limetokea jana majira ya saa nne za usiku baada ya Paulina Joseph na Noelia Abdallah ambao ni wake wa Chilanga Lwamba mwenye umri wa miaka 31 walipo kwenda nyumbani kwa Asteria Jailosi na kumkuta akishirikiana unyumba na mumewao.


Kutokana na tukio hilo wanawake hao walianza kumshambulia Asteria Chambulia kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha Noelia Abdallah akaamua kumng’ata mdomo wa chini kutokana na hasira aliyokuwa nayo.


Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo amesema tukio hilo ni la kushangaza kwa mwanaume huyo mwenye wake wawili kuamua kutafuta mwanamke mwingine

Post a Comment

 
Top