Menu
 

Na Shaban Kondo.
Chama cha wasioona Tanzania kipo kwenye mchakato wa kuanzisha mradi wa kiwanda cha kutengeneza fimbo zitakazotumiwa na walemavu wasiiona. Mkurugenzi wa Chama hicho James Shimwenye ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.Shemwenye amesema fimbo hizo zitasaidia kuwaongoza njia sanjari na jamii kuwatambua kwa haraka na kuwapatia msaada kama kuwavusha barabara.Amebainisha kuwa fimbo hizo pia zitasaidia kuwaepusha walemavu kuingia katika mashimo au kujigonga na vitu njiani kwa kuwa zitakuwa zikiwatambusha vitu vilivyopo mbele. Amesema ukosefu wa fimbo hizo ni sehemu ya changamoto kwa walemavu wa macho hasa wanapokuwa kwenye matembezi.Aidha amesema amesema fimbo nyeupe imetambuliwa rasmi kisheria katika sheria ya watu wenye ulemavu. Ameongeza kuwa hivi karibuni wanatarajia kufanya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kukarabati majengo ambayo yatatumika kwa shughuli za kiwanda hicho.

Post a Comment

 
Top