Menu
 


Christiano Ronaldo akiwa ameshika Kombe enzi akiichezea Manchester United.

Na Shaban Kondo.
  Nchini Uingereza:

Mtendaji mkuu wa klabu ya Man Utd David Gill ameshindwa kuficha hisia za klabu hiyo juu ya mshambuliaji kutoka nchini Ureno Cristiano Ronaldo ambae bado anaendelea kuhusishwa na mpango wa kurejea old Trafford.


David Gill ameshindwa kuficha hisia za kumuona mshambuliaji huyo akirejea katika himaya ya mashtamni wekundu, alipohojiwa na kituo cha televisheni cha Sky Sports ambapo amesema si vibaya endapo ropnaldo atarejea katika utawala wao.


Amesema Cristiano Ronaldohttp://static.lingospot.com/spot/image/spacer.gif ni mchezaji mzuri na mwenye hadhi ya kuitumikia klabu ay man utd ambayo ilimuuza mwaka 2009, baada ya kuonyesha uwezo mzuri ambao uliwavutia Real Madrid na kukubalia kutoa kiasi cha paund million 80 kama adayake ya uhamisho.


Gill amesema hatoshangazwa na mpango wa ronaldo endapo utatua mezani kwake kwa ajili ya kusajiliwa kwa mara nyingien tena, hivyo amesisitiza suala hilo kuachwa na kuamini bado mshambuliaji huyo ni bora kati ya wachezaji walio bora.


Katika hatua nyingine mtendaji mkuu wa klabu ya Man Utd David Gill akagusia suala la sakata la usajili wa winga kutoka nchini Uingereza na klabu ya Crystal Palace Wilfried Zaha kwa kusema hawajafanya bishara yoyote ya kmusajili mchezaji huyo.


Hata hivyo akatabiri kwamba Wilfried Zaha huenda akafanikisha dili la kusajili na klabu nyingine yoyote katika kipindi hiki kutokana na ubora wake.

Post a Comment

 
Top