Menu
 


 
 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dk.Norman Sigalla akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Habari kamili.
 Halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini imeanza mchakato wa kuanzisha benki ya wananchi benki ambayo inatarajiwa kuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima na wananchi wa kipato cha chini.Akiongea na wajumbe wa kamati ya mipango ya uanzishwaji wa benki hiyo Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dokta Norman Sigala amesema benki hiyo inatajiwa kuanzishwa ili kuwawezesha wananchi kukabiliana na matatizo ya kifedha.Aidha ametoa wito kwa wafanyabiashara kununua hisa za benki hiyo ili waweze kunufaika wao na familia zao kupitia benki yao.Nao wafanyabiashara walioshiriki kikao hicho wamesema changamoto kubwa ambayo wamekuwa wakikabiliana nayo ni maeneo maalumu kwa ajili ya kufanyia shughuli zao.

Post a Comment

 
Top