Menu
 

 
Wanafunzi wa shule ya msingi Nero Jijini Mbeya wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na hali ya vyoo wanavyotumia.

 Hayo wameyasema hii leo wakati walipokua wakizungumza na mwandishi wetu wamesema hali ya vyoo shuleni hapo ni mbaya kutokana na  kujaa kwa takribani miezi saba hali inayowafanya kujisaidia vichakani na wengine kujisaidia pembeni ya tundu la choo.

 Mmoja wa wanafunzi hao Memori Kiandu amesema wamekuwa wakisumbuliwa na hali hiyo licha ya kuchangia shilingi elfu tatu kwa ajili ya kujengewa vyoo vingine.

 Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Gasper Lyimo  amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema mamlaka husika isimamie suala hilo  kwani limedumu kwa muda mrefu.

 Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa wa Iyela Two Pipingu Mwakilasa amesema wameanza kujenga vyoo vingine kutokana na kujaribu kuzibua vyoo hivyo na kushindikana.

Post a Comment

 
Top