Menu
 Serena Williams katika pozi.
Katika Tennes:

Hofu imetanda juu ya hali ya mwanadada kutoka nchini Marekani Serena Jameca Williams ambae atashuka dimbani hapo leo kumkabili mpinzani wake kutoka nchini Marekani Sloane Stephens, baada ya kujitonesha maumivu ya kifundo cha mguu wakati akicheza mchezo wa wawili wawili kwa kushirikiana na dada yake Venus Williams hii leo.


Serena Williams alijitonesha maumivu ya kifundo cha mguu wake wa kulia, baada ya kuupinda mguu huo katika seti ya kwanza wakati akiwa katika harakati za kuucheza mpira uliokua umepigwa upande wao.


Hata hivyo pamoja na kuonekana kuupinda mguu huo, Serena alionekana amekunja uso kwa kuugulia machungu lakini, cha kushangaza aliendelea kabla ya kuutonesha tena mguu huo katika seti ya mwisho ambayo ilishuhudia wakipoteza kwa seti mbili kwa moja ambazo ni  tatu kwa moja ambazo ni  3-6, 7-6 na 7-5 dhidi ya Sara Errani na Roberta Vinci kutoka nchini Italia.


Sara Errani na Roberta Vinci sasa watakutana na Ekaterina Makarova ambae anaunda timu ya Urusi kwa kucheza na Elena Vensina katika mchezo wa hatua ya nusu fainali.

Post a Comment

 
Top