Menu
 


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya Diwani Athuman.


Jeshi la polisi mkoani Mbeya limezindua utaratibu mpya kwa kuhimarisha mawasiliano baina yake na wananchi kwa kuzindua namba mpya ya kutoa taarifa ndani ya jeshi hilo.Akizindua kampeni hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amesema kutokana na uchache wa askari waliopo mkoani hapa jamii haina budi kushirikiana na jeshi hilo ili kuimarisha ulinzi na amani.Aidha amewataka viongozi wa dini na wakisiasa kutoa elimu kwa jamii kuhusu polisi jamii ikiwa ni pamoja na kutoa maoni ndani ya jeshi badala ya kulalamika.Wakati huohuo ametoa wito kwa jamii kutoa maoni yao ya kweli ili kuboresha utendaji kazi na kwamba huduma hiyo itakuwa na usiri mkubwa na utafanyiwa kazi kwa muda mfupi.

Post a Comment

 
Top