Menu
 

Na Shaban Kondo.
 Kamati ya Utendaji ya Simba imepitia na kuidhinisha majina ya wajumbe wa kamati mbalimbali za klabu lengo likiwa kuiboresha klabu na pia kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara na michuano ya klabu bingwa Afrika itakayoanza mwezi ujao ambapo mabingwa hao wa tanzani bara watapambana na mabingwa kutoka nchini Angola Recreative de Libobo.Taarifa iliyotumwa na afisa habari wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga imeeleza kwamba mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Aden Rage, amewapongeza wote walioteuliwa kwa ajili ya kazi hiyo na kuwatakia mafanikio mema katika kuijenga klabu ili iwe ya kisasa kama walivyo wajumbe wenyewe.Kamati zilizoundwa na kamati ya utendaji ya klabu ya simba ni :KAMATI YA UFUNDI

 Damian Manembe (Mwenyekiti), Ibrahim Masoud (Makamu Mwenyekiti), Crescencius Magori, Khalid Abeid, Said Tully, Dr. Kategile, Zamoyoni Mogela, John William (Del Piero), Yusufu Macho, Jeff Lea, Bita John pamoja na Shabaan Baraza 


 KAMATI YA FEDHA

Geofrey Irick Nyange (Mwenyekiti), Rahma Al Khaloos (Makamu Mwenyekiti) Francis Waya, Zitto Kabwe, Juma Nkamia pamoja na Ruge Mutahaba


 KAMATI YA MASHINDANO

Swedy Mkwabi (Mwenyekiti), Said Pamba (Makamu Mwenyekiti) Selemani Zeddy. (Mb), Charles Hamkah, Said Rubeya, Abdulfatah Salum (Saphire), Hatibu Mwinyi (Busta) pamoja na Abdul  Mshangama.


Wengine ni Humphrey Zebedayo, Majaliwa Mbassa, Suleiman Zakazaka, Kesi Mohamed Rashid, Jerry Yambi, Iddi Kajuna, Chaurembo, Gerlad Lukumay, Habbib Nassa, Bundala Kabulwa, pamoja na Mohamed Issa Mbena


 KAMATI YA PROGRAMU ZA VIJANA

Ibarhim Masoud (Mwenyekiti), Ruge Mutahaba (Makamu Mwenyekiti) Joseph Itang’are-Mjumbe/Mlezi, Wilfred Kidau, Mohamed Abdallah, Said Tully, Canisius Masombola, Hamis Mrisho, Damas Ndumbaro Pamoja na Talib Hilal.


Uteuzi huo wa wajumbe unaanza mara moja na wenyeviti wa kamati hizo wamepewa nguvu ya kuitisha vikao vya kamati zao mapema iwezekanavyo.Wakati huo huo kikosi cha klabu ya Simba kinatarajia kurejea nchini kesho saa 10 jioni kutoka nchini Omani na kitaingia moja kwa moja kambini kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya mchgezo wa kwanza wa mzunguuko wa pili wa ligi kuu ya soka tanzani bara ambapo watapambana na African Lyon katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Post a Comment

 
Top