Menu
 


Jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kushuhudia ng'ombe huyo akiwa amefariki lakini hawakuchukua hatua zozote za kisheria dhidi ya mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein, aliyetumia gari lake kufanya mauaji ya ng'ombe huyo.(Picha na Maktaba yetu).
Habari kamili. 

Kesi inayowakabili wawekezaji wa Kapunga Rice Project dhidi ya wakulima wa kijiji cha Kapunga imeendelea katika mahakamu ya mkoa Mbeya ambapo wananchi wa kijiji jicho wameanza kutoa ushahidi wao.Kesi hiyo inayoendeshwa na Hakim mfawidhi wa mahakama hiyo Maiko Mteite huku wawekezaji hao wakitete na mwanasheria wa kujitegemea Radislaus Rwekaza wakati wakulima wao wakitete na wakili wa Serikali Achirey Mulisa ambapo kutokana na utata wa lugha wanayoitumia watuhumiwa na walalamikaji mahakama ililazimika kumtafuta mkarima wa lugha ya Kiingereza na Kiswahili kutoka chuo kikuu cha sheria Mzumbe Judith Kyamba.Asubuhi ya leo wakulima wawili wametoa ushahidi wao ambapo wamesema kutokana na kitendo cha mwekezaji huyo kumwagia sumu mashamba yao yenye zaidi heka 10 wameingia hasara ya mamilioni ya fedha.Kesi hiyo yenye namba 43 ya mwaka 2012 imefunguliwa na wakulima hao wa Kapunga huku wakiwatuhumu   meneja wa shirika, Afisa ughani na rubani wa Kapunga Rice Project na kwamba kesi hiyo itaendelea tena kesho asubuhi.

Post a Comment

 
Top