Menu
 


Habari na mwandishi wetu.
 Kikundi cha Wagumu kimepata zaidi ya shilingi milioni mbili na elfu ishirini na nne huku kikiwa kimetimiza miezi mitatu tangu kuanzishwa kwake.Akiongea na mwandishi wetu katibu wa kikundi hicho Dokta Richard Magawa amesema kikundi hicho kinajumla ya wanachama kumi na moja ambapo mwanachama wa kikundi hicho huchangia shilingi elfu mbili kila siku ili kuujenga umoja wao.Amesema kati ya fedha hizo walizopata wanakikundi wamekubaliana kununua pikipiki moja yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nne kwa lengo la kuongoza kipato umoja na wanakikundi wenyewe.Aidha wametoa ombi kwa viongozi wa kiserikali kukisaidia kikundi hicho dhana za kilimo ili kuwawezesha kufanya kujiendeleza zaidi katika kilimo.

Post a Comment

 
Top