Menu
 

Tukio 1....

ATHARI ZILIZOJITOKEZA BAADA YA MWEKEZAJI WA KAPUNGA RICE PROJECT KUMWAGA SUMU.

Mguu ya Bwana Benjamini Hebel (44) mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kapunga, wilaya ya Mbrani mkoa wa Mbeya ilivyoharibika baada ya Mwekezaji wa Kapunga Rice Project Bwana Wally Vermaak. kumwaga sumu kwa kutumia ndege katika mashamba ya wananchi kufutia mgogoro wa kugombania ardhi baina ya wananchi na mwekezaji huyo.
 
 Baadhi ya wananchi walioathirika na Sumu iliyomwagwa na Mwekezaji Bwana Wally Vermaak. katika mashamba yao, na kisha kula mboga iliyomwagiwa sumu, hali iliyopelekea kuhara.
 Kibanda hiki nacho kilimwagiwa sumu na mwekezaji wa Kapunga Rice Project Bwana Wally Vermaak. licha ya wananchi kujihifadhi ndani ya kibanda hicho.
 Sehemu ya mimea ya mpunga na mahindi iliyonyauka katika mashamba ya wananchi wa Kijiji cha Kapunga baada ya kumwagiwa sumu na Mwekezaji wa Kapunga rice Project Bwana Wally Vermaak. .
  Sehemu ya mimea ya  mahindi iliyonyauka katika mashamba ya wananchi wa Kijiji cha Kapunga baada ya kumwagiwa sumu na Mwekezaji wa Kapunga rice Project Bwana Wally Vermaak..
 Mtoto huyu alikuwepo shambani wakati mwekezaji akimwaga sumu mashambani.
  Sehemu ya mimea ya mpunga na mahindi iliyonyauka katika mashamba ya wananchi wa Kijiji cha Kapunga baada ya kumwagiwa sumu na Mwekezaji wa Kapunga rice Project Bwana Wally Vermaak..
  Sehemu ya mimea ya mpunga na mahindi iliyonyauka katika mashamba ya wananchi wa Kijiji cha Kapunga baada ya kumwagiwa sumu na Mwekezaji wa Kapunga rice Project Bwana Wally Vermaak.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kapunga Bwana Ramadhani Nyoni akionesha turubai ambalo lilitumika kufunika mbegu na kisha kunyunyiziwa sumu ambayo iliharibu turubai hilo na mbegu. (Picha na Ezekiel Kamanga).
Tukio 2.....
 

VURUGU ZA MWEKEZAJI WA KAPUNGA RICE PROJECT (KRP) MBARALI NI TETE

Mfugaji Bwana Mungo Makubi (27) kushoto na Singu Mwakami (23) wakimtazama ng'ombe aliyeuawa kwa kugongwa na gari aina ya Toyota Landcruiser lenye nambari ya usajili T 566 BQH. iliyokuwa ikiendeshwa na mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein baada ya kuwakosa wafugaji hao baada ya kujistiri nyuma ya mti na kisha hasira za mwekezaji kuishia kwa kumgonga ng'ombe huyo mwenye thamani ya shilingi laki 6 za kitanzania na kisha kufa papo hapo.
Gari aina ya Toyota Landcruiser lenye nambari ya usajili T 566 BQH. iliyokuwa ikiendeshwa na mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein na kisha kumgonga ng'ombe mwenye thamani ya laki 6 na kisha kufa papo hapo, baada ya kuwakosa wafugaji hao baada ya kujistiri nyuma mti.
Jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kushuhudia ng'ombe huyo akiwa amefariki lakini hawakuchukua hatua zozote za kisheria dhidi ya mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein, aliyetumia gari lake kufanya mauaji ya ng'ombe huyo.
Wafugaji wakionesha jinsi mwekezaji huyo alivyokuwa akiwakimbiza na pichani ni alama za magurudumu ya gari yalipopita wakati akiwafukuza.
Sehemu ya shamba ambayo mwekezaji wa Kapunga Rice Project ameshindwa kuilima na nyasi zikiendelea kuota.
Moja ya mitambo inayotumika katika shughuli katika shamba hilo la Kapunga Rice Project ikiwa imeachwa katika moja ya sehemu ya shamba ambayo mwekezaji ameshindwa kuilima, na nyasi kuendelea kuota.
Baada ya mwekezaji wa Kapunga Rice Project kufunga njia zinazoingia na kutoka, pia kufunga maji ya bomba wananchi wa kijiji cha Kapunga wapo katika hatari kubwa kama inavyooneka pichani, wanawake wakivuka kuelekea ng'ambo ya pili kwa kutumia gogo.
(Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya)

Post a Comment

 
Top