Menu
 

Na Shaban Nassoro.
Serikali ya nchi za Hongkong na China zipo katika hatua za awali ilikufanya makubaliano ya wafanyabiashara ya nyama kutoka nchini Tanzania kupitia Kampuni ya ranchi ya taifa NARCO.

Akizungumza na Kituo hiki jijini Dar es Salaam Afisa masoko wa kampuni ya NARCO Immanuel Mzava amesema nchi hizo za Hongkong na China zinahitaji tani 75 za nyama ya ng’ombe ambazo zitakuwa zikiuzwa kupitia TMC katika kipindi cha mwezi mmoja ujao.

Amesema kutokana ukubwa wa soko hilo NARCO inafanya mazungumzo na TMC kuangalia uwezekano wa kuboresha baadhi ya vitendea kazi na mfumo wa upozeshaji ili kuweza kumudu ukubwa wa soko hilo.

Amesema soko hilo pia litahitaji vifaa kama pembe, kwato, maini, ngozi na utumbo ambao utasafirishwa katika matunzo maalumu ikiwa ni sehemu ya oda ya soko hilo.

Hatahivyo ndugu Mzava amewataka wadau mbali mbali ufugaji ng’ombe kutoa ushirikiano wa kupeleka ng’ombe ili kutosheleza soko hilo la nyama ikiwa ni pamoja na mazungumzo yanaendelea kupata wakala atakayeuza Kongwa beef Dodoma mjini ili kuongeza mauzo ya ndani.

Ametaja masoko mengine la ndani kuwa ni pamoja na nchi za Zambia ambalo tayari wameanza kupelekewa nyama ya ng’ombe 1000 wamechinjwa kupitia SAAFI na kuuzwa nje ya nchi na Zambia.

Aidha akizungumia soko la ndani amesema NARCO amejipanga kufungua kituo cha mauzo Morogoro nanenane haraka iwezekanavyo ili kuongeza mauzo ndani ikiwa ni pamoja na kufungua bucha Mwenge, Mikocheni na Mbezi Beach.

Post a Comment

 
Top