Menu
 

 Meya wa Jiji la Mbeya  Athanasi Kapunga,

Chanzo Bomba FM, Mbeya.
Mstahiki meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga  amesema  kumekua na  tabia ya  kuwepo msongamano wa abiria katika vituo vya mabasi yaendayo mikoani visivyo rasmi hasa kituo kidogo cha magari eneo la Mwanjelwa.

Akizungumza na Bomba FM amesema kuwa halmashauri ya jiji  imejipanga kushughulikia suala hilo na wana mikakati juu ya kulijenga jiji la Mbeya.

Amesema halmashauri ya jiji la Mbeya imedhamiria kuzirekebisha barabara zote kwa kiwango cha lami ambapo kila mwaka halmashauri itakuwa ikijenga barabara zenye urefu wa kilometa 10.

Aidha amesema ili kukabiliana na msongamano wa magari kati kati ya Jiji Halmashauri imedhamiria ya kujenga vituo vya mabasi yaendayo wilayani mwanzoni mwa mji.

Kapunga  amekiri  kuwa utaratibu wa sasa wa mipango miji si mzuri na halmashauri hiyo imejipanga katika mipango hiyo  ikiwa na nia ya kuboresha barabara za mitaa ili kupunguza vituo vya mabasi visivyo rasmi.  

Hata hivyo amekemea vikali vitendo vya  madereva ambao wamekuwa wakitoka eneo la stendi kuu na kuifanya stendi eneo la Mwanjelwa ambalo si rasmi kwa mabasi yaendayo  mikoani.

 Wakati huohuo ametoa wito kwa taasisi za kibenki kuanza kuangalia namna ya kujenga ofisi zao pembezoni mwa mji ili kurahisisha huduma kwa wananchi wanaolazimka kuja mjini kuzifuata

Post a Comment

 
Top