Menu
 


Real Madrid HD wallpaper for Wide 16:10 5:3 Widescreen WHXGA WQXGA WUXGA WXGA WGA ; HD 16:9 High Definition WQHD QWXGA 1080p 900p 720p QHD nHD ; Other 3:2 DVGA HVGA HQVGA devices ( Apple PowerBook G4 iPhone 4 3G 3GS iPod Touch ) ; Mobile WVGA iPhone PSP - WVGA WQVGA Smartphone ( HTC Samsung Sony Ericsson LG Vertu MIO ) HVGA Smartphone ( Apple iPhone iPod BlackBerry HTC Samsung Nokia ) Sony PSP Zune HD Zen ; 
Na Shaban Kondo.
 Mabingwa wa soka nchini Hispania Real Madrid  wameendelea kuongoza katika orodha ya vilabu vinavyoingiza fedha nyingi zaidi duniani baada ya kuwa klabu ya kwanza ya michezo kuingiza kiasi cha euro milioni 500 kwa msimu mmoja.


Mapato hayo ambayo yamepatikana ndani ya klabu hiyo katika msimu wa mwaka 2011-2012 yanaifanya klabu hiyo kuongoza kwenye orodha ya misimu minane mfululizo wakifuatiwa na mahasimu wao FC Barcelona ambao wameingiza kiasi cha euro milioni 483.


Nafasi ya tatu katika orodha hiyo imeshikwa na klabu ya Manchester United ambayo imeingia kiasi cha euro milioni 395.9 wakifuatiwa na klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujetumani  ambayo imeingiza kiasi cha euro milioni 368.4 huku ya nafasio ya tano ikichukuliwa na klabu ya Chelsea ambayo imeingiza kiasi cha euro milioni 322.6.


Washika bunduki wa Ashburton Grove, Arsenal wameporomoka kwa nafasi mbili kutoka katika nafasi ya nne hadi katika nafasi ya sita katika orodha hiyo ambapo kwa msimu uliopita wamefanikiwa kuingia kiasi cha euro milioni 290.3.


Mabingwa wa soka nchini Uingereza Manchester City wamepanda hadi katika nafasi ya saba kwa kuingiza kiasi cha euro milioni 285.6 msimu uliopita, wakifuatiwa na AC Milan walioingiza kiasi cha Euro million 256.9.


Kwa upande wa majogoo wa jiji Liverpool wao wameshika nafasi ya tisa kwa kuingiza kiasi cha cha euro 233.2 na katika nafasi ya kumi wapo mabingwa wa soka nchini Italia Juventus walioingiza kiasi cha euro 195.4

Post a Comment

 
Top