Menu
 
Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki imeahidi kuendelea kuunga mkono michezo ikiwa ni pamoja na kukarabati miundombinu ya viwanja vya michezo.

Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda ametoa uhakika huo hii wakati alipofungua michuano ya ya kanda ya tano ya mpira wa kikapu inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini kwa kushirikisha timu 13 kutoka kwenye mataifa saba.


Kwa upande wa rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Nchini (TBF) Musa Mziya ameiomba Serikali iangalie kwa macho mawili swala la miundombinu la viwanja vinavyokidhi hadhi ya mashindano makubwa kama hayo.

Katika mchezo wa awali kwa upande wa Wanawake timu ya Tanzania 'Tanzanite Queens' ilianza vibaya michuano hiyo kwa kufungwa kwa pointi 74 - 32 na timu ya Kenya katika mchezo ambao Tanzanite ilionekana kuzidiwa kila idara kutokana na wachezaji wa Kenya kuwa warefu.

Nchi zinazoshiriki katika mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Misri, Burundi na Somalia.
Bingwa wa michuano hiyo atawakilisha nchi yake katika mashindano ya Afrika yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA).

Post a Comment

 
Top