Menu
 

Andrés Iniesta Luján

 Kiungo aliewezesha timu ya taifa ya Hispania kutwaa ubingwa wa kombe la dunia mwaka 2010, Andrés Iniesta Luján amesema hana mpango wa kuihama klabu ya Barcelona na badala tyake amejiwekea matarajio ya kumaliza soka lake akiwa na klabu hiyo iliyomkuza tangu akiwa na umri mdogo.


Andres Iniesta mwenye umri wa miaka 28, tayari ameshacheza michezo zaidi ya 400  katika kikosi cha kwanza cha FC Barcelona tangua lipopandishwa katika kikosi hicho akitokea kwenye shule ya kukuzia vipaji ya Lamasia, amebainisha mpango huo kufuatia sakatala la baadhi ya wachezaji kuanza kuhisiwa huenda wakaondoka Camp Nou.


Amesema nia yake ni kuitumikia klabu hiyo inayoongoza kwenye mnsimamo wa ligi ya nchini Hispania kwa sasa mpaka atakapoamua kuachana na soka, huku sababu nyingine aliyoitaja ni kuuzwa na uongozi wa klabu hiyo kama itatokea huko mbele ya safari.


Andres Iniesta pia akakiri kwamba FC Barcelona kwa sasa wanakabiliwa na wakati mgumu baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi msdimu huu, lakini akawasihi wachezaji wenzake kuhakikisha wanarejesha akili zao mchezoni kabla ya kucheza mchezo wa kombe la mfalme dhidi ya Malaga sutakaochezwa siku ya Al-khamis katika uwanja wa La Rosaleda


Kwa mara ya kwanza msimu huu FC Barcelona walikubali kupoteza mchezo kwa kukubali kichapo cha mabao matatu kwa mawili dhidi ya Real Sociedad. 

Post a Comment

 
Top