Menu
 

 
 Wesley Sneijder
Na Shaban Kondo
Klabu ya Galatasaray  imefanikiwa kumnasa kiungo kutoka nchini Uholanzi, Wesley Sneijder kwa ada uhamisho ya euro milioni 7.5 kutoka kwenye klabu ya Inter Milan ya nchini Italia.

Klabu ya Galatasaray yenye maskani yake Türk Telekom Arena mjini Istanbul nchini Uturuki imetoa taarifa za kumsainisha nyota huyo mkataba wa wa miaka mitatu ambao utamuwezesha kuwepo klabuni hapo hadi mwaka 2016.

Sneijder alijiunga na klabu ya Inter Milan mwaka 2009 akitokea kwenye klabu ya Real Madrid mwaka 2009 na alikuwa mmojaw a wachezaji walioiwezesha klabu hiyo ya mjini Milan kutwaa taji la Serie A msimu wa mwaka  2009–10 pamoja na taji la Coppa Italia katika msimu wa mwaka  2009–10 na 2010–11.

Mataji mengine yaliyochukuliwa huko Stadio Guissepe Meaza wakati kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 ni Super coppa Italiana mwaka  2010, ligi ya mabingw abarani ulaya msimu wa mwaka 2009–10 pamoja na klabu bingwa duniani mwaka  2010

Tukiwa bado mjini Milan, nchini Italia:
Klabu ya AC Milan inapanga kuuwahi muda wa usajili wa majira ya baridi utakaofikia kikomo Januari 31, kwa kuhakikisha wanamrejesha kiungo kutoka nchini Brazil Ricardo Kaka.

Ricardo Kaka mwenye umri wa miaka 30 aliondoka Milan mwaka 2009 baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa muda wa misimu sita na kujiunga na klabu ya Real Madrid ambayo kwa sasa imekua ikimpa wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Post a Comment

 
Top